WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
KAMA ULIKUWA UNASUBIRI MECHI YA SIMBA NA YANGA, KUNA MABADILIKO HAYA
Na Dina Ismail, DAR ES SALAAM
MECHI ya watani wa jadi, Simba SC na Yanga SC mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyokuwa ichezwe Oktoba 12, mwaka huu imefutwa na sasa tarehe mpya itatajwa kesho.
MECHI ya watani wa jadi, Simba SC na Yanga SC mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iliyokuwa ichezwe Oktoba 12, mwaka huu imefutwa na sasa tarehe mpya itatajwa kesho.
Taarifa ya TFF leo imesema kwamba, hiyo iantokana na mchezo wa kirafiki wa
kimataifa baina ya Taifa Stars na Benin ambao kwa ujumla utabadilisha ratiba ya
Ligi Kuu na marekebisho hayo yatatangazwa kesho (Septemba 26 mwaka huu).
Taifa Stars inashuka uwanjani Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi
ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa baadaye na Kocha
Mkuu Mart Nooij.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaendelea na taratibu nyingine kwa ajili ya
mechi hiyo ikiwemo usafiri wa Benin kuja nchini, ambapo timu hiyo inatarajiwa
kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Oktoba 10 mwaka
huu ikiwa na msafara wa watu 28.
Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha
Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha
upendo kati ya
viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu.
Wakati huo huo: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajia kufunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara.
Wakati huo huo: Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatarajia kufunga mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa vyama vya mpira wa miguu wa wanawake vya mikoa ya Tanzania Bara.
Hafla ya kufunga mafunzo hayo itafanyika kesho (Septemba 26 mwaka huu) saa 5
asubuhi kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Mafunzo hayo ya siku tano yalishirikisha viongozi 34 wakiwemo baadhi ya
waandishi wa habari na Meneja wa Twiga Stars, na yaliendeshwa na Mkufunzi wa
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau.
RAIS KIKWETE ANAHITAJIKA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI
KUTOKA Arusha, TANZANIA
Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa mashahidi wanaotarajiwa
kuitwa na walalamikaji katika shauri dhidi ya nchi za Kenya, Uganda na Rwanda
linaloendelea katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ).
Wakili Jimmy Obeid anayewawakilisha walalamikaji katika shauri
namba 9/2013, jana aliieleza Mahakama kuwa miongoni mwa mashahidi watakaoitwa
kujenga kesi hiyo ni pamoja na Rais Kikwete.
Shauri hilo lilifungulliwa na Watanzania watatu, Ally Hatib
Msangi, David Makatha na John Bwenda wakidai kitendo cha Kenya, Uganda na
Rwanda kufanya vikao bila kuzishirikisha Tanzania na Burundi ni ukiukwaji wa
mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Miongoni mwa vifungu vya mkataba wa EAC vinavyodaiwa kukiukwa ni
namba 3(3) (c) kinachotaka ushiriki sahihi kuimarisha ushirikiano ndani ya
ukanda wa Afrika Mashariki na Kifungu cha 6 (a) (b) (d) na (f) kinachozitaka
nchi wanachama kuzingatia misingi ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.
Katika ushahidi wake, Rais Kikwete ataombwa kuthibitisha hotuba
yake kwa Taifa aliyoitoa bungeni Novemba 7, mwaka jana ambayo ilielezea jinsi
Tanzania na Burundi zilivyotengwa na baadhi ya nchi wanachama wa EAC.
“Kutokana na uzito na majukumu ya Rais Kikwete tunayepanga
kumwita kama mmoja wa mashahidi wetu, naiomba Mahakama muda wa mwezi mmoja
kuwasilisha orodha ya mashahidi na hati za viapo,” alisema Obeid. Jopo la
majaji watano wakiongozwa na Jaji Kiongozi, Jean-Bosco Butasi, Naibu Jaji
Kiongozi, Isaac Lenaola na wengine Faustin Ntezilyayo, Monica Mugenyi na Fakhi
Jundu walikubali ombi hilo na kupanga Oktoba 24, mwaka huu wadai kuwasilisha
hati ya kiapo na orodha ya mashahidi.
Wadaiwa katika shauri hilo ni Katibu Mkuu wa EAC,
anayewakilishwa na wakili Dk Antony Kafumbe wakati mdaiwa wa pili ni
Mwanasheria Mkuu wa Kenya anayewakilishwa na mawakili wawili, Muthoni Kimani na
Peter Ngumi, mdaiwa wa tatu ni Mwanasheria Mkuu wa Uganda anayewakilishwa na
mawakili watatu, Elisha Bafirawala, Richard Adrole na Maureen Ijang’ na mdaiwa
wa nne ni Mwanasheria Mkuu wa Rwanda anayewakilishwa na wakili Malaala Aimable.
Wadaiwa hao watawasilisha majibu kabla ya Novemba 7 mwaka huu na
kutoa maelezo ya ziada Novemba 14 mwaka huu kabla ya Mahakama kupanga siku ya
shauri hilo kusikilizwa na pande zote zitapewa wito maalumu.
Septemba 2, mwaka huu, wadai waliondoa mahakamani ombi la zuio
la muda dhidi ya vikao vya muungano wa wenye nia (coalition of the willing),
baada ya Tanzania na Burundi kuanza kushirikishwa kwenye vikao viwili
vilivyofanyika Februari 24 na Mei 2, mwaka huu.
DAH: MKE WA WIZ KHALIFA, AMBER ROSE, AFUNGUA MADAI YA TALAKA…..INASEMEKANA NICK CANNON NDIYE CHANZO
LOS ANGELS, Marekani
BIG News
nay a kushtua ni hii ambayo TTM tumekutana nayo ikizunguka kunako Mitandao
Mbali mbali ya Kijamii, kuhusu Kuvunjika kwa Ndoa ya Amber Rose na Wiz Khalifa,
iliyodumu kwa Muda wa Mwaka 1 na Miezi kadhaa..FULL STORY iko Hivi…
Mpaka Hivi
sasa, tayari Amber Rose ameshafungua jalada la Kudai talaka kutoka kwa Mumewe
Huyo CAMERON THOMAZ, maarufu kama Wiz Khalifa.
Ingawa
Mpka hivi sasa Wiz Khalifa hajatoa Taarifa Maalum kuhusu chanzo cha wawili hao
Kutemana, Lakini huwezi amini, tatizo kubwa linaloonekana kuwepo, Ni Usaliti
baina ya wanandoa hao wawili, ambapo kila mmoja anamlaumu mwenzake kwa
Kujihusisha na UCHEPUKAJI mkubwa.
Licha ya
Miezi kuadhaa Amber Rose kupost Picha ya Ndoa yao, wakipongezana kwa Kutimiza
Mwaka Mmoja katika Ndoa yao, lakini hivi sasa Ni KWISHA HABARI, hakuna cha
Amber Rose , wala Wiz Khalifa Kuhusiana na Ndoa.
·
Ugomvi Ni Mkubwa:
Kama
Ilivyokuwa kwa Nick Cannon na Mariah Carey, basi safari hii imekuwa hivyo Hivyo
kwa upande wa Wiz Khalifa ambaye anafanya Vema na Albam Yake ya BLACCHOLLYWOOD
iliyosheheni mangoma Makali likiwemo la WE DEM BOYS. Chanzo kilicho karibu na
wawili hao, kinadai kuwa, Ugomvi ulioko baina ya wanandoa hawa wawili, ni
Mkubwa na Mchungu , maana hata ukiangalia Documents za kudai talaka, ni Chungu
balaa
·
Nick Cannon Kuhusika Katika Kuvunjika Kwa Ndoa
Hiyo.
Hivi
majuzi tu, Aliyekuwa Mume wa Mariah Carey, Nick Cannon ambaye nayeye Ndoa yake
iliingia katika Noma Kubwa na Madai ya talaka Kufunguliwa, alisikika akisema
kuwa, anataka kumfanya Amber Rose awe Maarufu kupitia Televisheni na Huenda
akashirikiana naye hasa Kibiashara.
Kauli hiyo
iliwafanya wengi wajiulize maswali, hasa ukizingatia inasemekana kuwa Eti,
Amber Rose na Nick Cannon wameshawahi kushiriki katika Mkunjuko wa Kimapenzi.
Hali Hiyo
ilizua Utata sana, huku wanahabari wakidhani kuwa huenda Nick cannon anazingua,
lakini walipomhoji Amber, alikiri kuwa ni Kweli, atafanya kazi na Nick Cannon,
·
Nick Cannon Amejibu Hivi:
Kwa upande
wake Nic Cannon ambaye kwa asilimia kubwa ni HOST katika Vipindi mbali mbali
hasa AMERICA HAS GOT TALENT, amesema kuwa yeye hajahusika kwa namna yoyote ile,
katika kuvunjika kwa Ndoa ya Wiz khalifa na Amber Rose
Pia Cannon
ameongeza ya kwamba, Yeye na Amber Rose, walikubaliana wafanye Mishe za
kibiashara tu, na hakuna ushauri wa kudai talaka uliotoka kwake hata Siku moja.
Fahamu Haya Machache:
- · Kipindi cha Awali, Amber Rose amewahi kuwa STRIPPER, yaani Mcheza Utupu/Uchi wa Night Clubs
- · Amewahi kukunjuka na Rapper Kanye West ingawa hawakudumu sana katika Mahusiano yao, huku ikiaminika kuwa Kanye alikuwa akigawa kifinyo kwa Amber Rose
- · Amber Rose aliwahi kumzawadia WIZ KHALIFA saa yenye Thamani kubwa, aliyowahi kupewa na Kanye West wakati wapo Katika mahusiano.
- · Amber Rose anataka apewe haki za malezi na Usimamizi wa Mtoto wao, SEBASTIAN THOMAZ “The Bash”, na anataka Wiz Khalifa awe anamtembelea Tu. Mtoto wao ana Umri wa Mwaka mmoja
“ADAM JUMA ANALIPWA VILE VILE,YAANI ANLIPWA KAWAIDA..ILA TUANGALIE AMETUTOA WAPI”-KAULI YA RIC MAVOKO
DAR ES SALAAM, Tanzania
NI KWELI Kipindi cha Nyuma Video
kali kama Vile, SHE GOTTA GWAN ya Ngwea, ICE CREAM ya Noorah, CHUNGWA ya
Suma-Lee na Nyinginezo kibao, tulikuwa
tunazielewa na kuzipenda sana kupitia mkono wa ADAM JUMA wa VISUAL LAB
SASA, Muimbaji na Mkali wa FOLLOW ME
ambaye Soon anaaachia mzigo Mpya wa PACHA WANGU, Rich Mavoko, amewasihi wasanii
wa Tanzania kukumbuka Mchango wa Adam Juma hasa pale walipo hivi sasa, na Kiasi
wanachomlipa.
Akizungumza kuhusiana na Hilo,
MAVOCO amesema kuwa, wasanii hawatakiwi kulalamika juu Adam Juma kuhitaji
Mkwanja Mrefu kufanya Video, pasipo kukumbuka Mchango wake katika Video
Industry hapa Nchini Tanzania
Hapa Tunamnukuu akisema:
“Lakini tuangalie pia ametutoa wapi. Movement
zake kuhusu music video Adam Juma ameitoa wapi. Tuapreciate kitu ambacho
amekifanya. Mimi naweza nika-appreciate media, maDj, na wasanii wenzangu basi
tuapreciate pia (Adam J) ametutoa mbali ujue.”
Tofauti na hilo, Rich Mavoco
ameongeza kuwa mpaka hivi sasa, kwa asilimia kubwa Adam Juma analipwa Kawaida,
na Analipwa Vile Vile.
Aidha kuhusu Video yake hiyo Mpya,
mavoko amedai kuwa, adam Juma na Timu yake Nzima, walisafiri Mpaka Cape Town,
na wametumia Vifaa vya Kisasa, huku kazi Nzima ikifanyikia huko huko Afrika ya
Kusini.
Adam Juma amewahi Kutengeneza Hit
Songs za wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya ambao Hivi sasa wamekimbilia
Production za Kimataifa kama Vile OMMY DIMPOZ (Nai Nai & Baadaye) pamoja na
DAIMONDS ( Kamwambie , Mawazo,Mbagala , nitarejea & Moyo wangu)
SHAVU KWA SHAVU: DIAMONDZ PLATNUMZ APATA UBALOZI, YOUNG DEE APATA UBALOZI..
DAR
ES SALAAM, Tanzania
WAKATI Diamonds akitoa tamko Rasmi
kuhusu Kuwa balozi wa Application ya MZIIK hasa kunako SMART PHONES, Muda huo
Huo pia tukapata Info kuwa YOUNG DEE naye karamba Ubalozi wa Channel moja hivi
ya kampuni ya STAR TIMES..sasa Hii ni Kupitia Account zao za Instagram
·
Kwa Upande
Wa Diamondz “Dangote”
“Chibu Dangote” ama Nasib Abdul
alikutana na Shavu la kutosha kwa Kuwa Balozi wa Application Mpya ya Simu za
aina ya Smart Phones, inayoitwa MZIIKI.
Hapa tunanukuu Kauli yake
“Ningependa kukutaarifu Shabiki
yangu Mpendwa kuwa, Kijana Wako sasa Ni balozi wa Application Mpya iitwayo
#MZIIKI
Akamaliza Chib dangote huku kwa Chini
akiitafsiri kwa Lugha ya Kiingereza kwa wale wasiofahamu Kiswahili
·
Kwa Upande
Wa Young Dee
Naye rapper Young Dee ambaye hivi
sasa anafanya Poa na Mkwaju mpya wa SIO MCHOYO, naye alitoa Mtonyo kuwa ni
Baalozi wa Channel ya Q-YOU ya Star Times….hapa tunamnukuu
“Thanks #StarTimes for Such a
Deal…..New Ambassador of #Qyou Chanel….. Its Official Now
Kwa Upande wetu TTM, tunawatakia
kazi Njema, hasa katika kutangaza Bidhaa walizokabidhiwa. Ameeen
10 Healthy and Delicious Avocado Recipes
PURHIYA Mahmoud
Last year it was made the first homemade bread
from one of the favourite banana recipes. It was so delicious! And now, Now,
its better we show you how to make the
first avocado recipe with walnut bread. we like avocados and some of people
like walnuts, so we believe it’ll be perfect dish for us.
Ingredients:
- 1
cup organic white, unbleached spelt flour
- 3/4
cup organic whole spelt flour
- 1
tsp baking powder
- 1/2
tsp bicarbonate of soda
- pinch
of salt
- 4
large free-range eggs
- 1/2
cup organic fat-free yoghurt
- 1
avocado, mashed
- 3
tbsp walnut oil
- 1
cup walnuts, chopped
Directions:
Preheat oven to 1800 C and prepare a standard
size loaf tin.
In a medium bowl, sift together the flours,
baking powder, bicarbonate of soda and salt. Beat the eggs in another bowl and
beat in the yoghurt avocado and oil. Fold the dry ingredients into the egg
mixture, add the walnuts and fold to combine. Bake for 45 minutes or until a
skewer inserted in the middle comes out clean.
Wonton cups with avocado and smoked salmon would
be a perfect appetizer during the party or holiday dinner. Bake this little
wonton cups inside mini muffin trays. When won ton cups come out of the oven,
they’ll have perfect little form to hold the ingredients of this delicious
avocado recipe.
Ingredients:
- 24
square won ton or shumai (dumpling) wrappers
- 2
tablespoons unsalted butter, melted
- 2
teaspoons white sesame seeds
- 4
ounces hot-smoked salmon (see Notes), flaked into small pieces
- 1/2
cup finely sliced green onions, including tops
- 1/4
cup finely chopped fresh cilantro
- 1
tablespoon lime juice
- 2
teaspoons grated fresh ginger
- 1/2
teaspoon kosher salt
- 1
small avocado, finely diced
Directions:
Preheat oven to 350° C. Lay 12 won ton wrappers
flat and, using about half the butter, brush both sides. Press into mini muffin
cups (2 tbsp. size), pleating each to form a small cup. Sprinkle wrappers with
half the sesame seeds. Bake until golden brown (watching carefully; they can
burn easily), 7 to 9 minutes. Loosen from cups with a small spatula and put on
a cooling rack. Repeat with remaining 12 won ton wrappers, butter, and sesame
seeds.
In a small bowl, combine salmon, green onions,
cilantro, lime juice, ginger, and salt; mix well. Add avocado and toss very
gently until well combined. Put a generous spoonful in each won ton cup. Serve
immediately.
HIVI NDIVYO FEDHA ZINAVYOMGONGANISHA SAMUEL SITTA NA KATIBU WAKE
Dodoma.TANZANIA
Kauli ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,
Samuel Sitta kwamba fedha ambazo
zitakuwa zimeokolewa katika siku 60 za uendeshaji wa Bunge hilo hazitarejeshwa
serikalini, bali zitatafutiwa utaratibu wa namna ya kuzitumia, imemgonganisha
na katibu wake, Yahya Khamis Hamad ambaye amesema “hilo ni jambo la ajabu”.
Sitta alitoa kauli hiyo juzi usiku wakati
akiahirisha Bunge hilo lenye wajumbe 500 baada ya wajumbe 130 wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) kulisusia tangu Aprili 16, mwaka huu.
Wajumbe hao wamekuwa wakilipwa posho ya Sh300,000
kwa siku sawa na Sh150 milioni kwa siku kwa wajumbe wote, huku Serikali ikiwa
imetenga Sh20 bilioni kwa ajili ya siku 60 za uendeshaji wa Bunge hilo.
Kauli hiyo ya Sitta kuwa fedha zitakazookolewa
zitatafutiwa utaratibu badala ya kurudishwa zilikotoka, iliwafanya wajumbe wa
Bunge hilo kulipuka kwa furaha na kugonga meza.
Hata hivyo, katibu wa Bunge, Yahya Khamis Hamad
alishangazwa na kauli hiyo ya Sitta akisema: “Mimi hayo niliyasikia lakini
kwangu pia ni ya ajabu kwa sababu fedha tulizonazo hazitoshi, sasa hizo za
kubaki mimi sijui.”
Katibu huyo alisema kwa sasa, Wizara ya Fedha
inawapa kiasi cha fedha kwa kile tu ambacho kinahitajika na yeye anatoa taarifa
serikalini kwa kiasi kilichotumika. “Mimi sijui labda yeye anajua sitaki
kumsemea,” alisema.
Sitta pia aliwaeleza wajumbe hao kuwa baada ya
kukabidhi Katiba inayopendekezwa, wote watakabidhiwa cheti na Rais Jakaya
Kikwete.
“Cheti hicho kitakuwa na sahihi ya Rais mwenyewe
kwa hiyo tutakaa kidogo kusubirisubiri Katiba iliyokamilika, haiwezi kuwa ya ovyo
ovyo tu lazima iwe na viwango vizuri,” alisema Sitta na kuongeza:
“Tutachapisha nakala nyingi kila mmoja aende na
waraka huo wa kihistoria nyumbani na itakuwa ni Katiba bora sana hapa Afrika na
Kusini mwa Sahara.”
Mwenyekiti huyo aliwapiga vijembe viongozi wa
Ukawa na makundi mengine yanayopaza sauti kutaka Bunge hilo lisitishwe ili
kuokoa pesa
“Tutamaliza zoezi hilo Oktoba 3, mwaka huu ili
tutoke na Katiba inayopendekezwa kinyume na wale wanaopiga kelele ovyo bila
kuwa na sayansi kichwani eti unaokoa gharama kwa kusitisha mchakato.
“Mchakato huu ungesitishwa ina maana utawala
ujao, rais ajaye ingembidi kuanza upya na Tume na aingie tena kwenye Bunge
Maalumu la Katiba,” alisema Sitta.
Subscribe to:
Posts (Atom)