R.KELLY aliyewahi
kuusumbua Ulimwengu wa R&B kipindi kileeee..na hivi sasa amekuwa ni
Zilipendwa, yuko katika Kuti kavu la Kushtakiwa na aliyekuwa Meneja wake
kipindi anapiga Mzigo
TTM tumeshushiwa
Ripoti na Kitengo Chimbua Chimbua, Mwaka jana, Robert Kelly aliyevunja hasa na
Kwaju la STORM IS OVER, alipigana Chini na manager wake, DERREL McDAVID, ambaye
amedumu naye Miaka na Miaka
Sasa Ripoti hiyo
inazidi kujieleza kuwa, Meneja huyo mstaafu, ameamua kufungua mashtaka Dhidi ya
Mkali huyo wa kitambo. Kwa madai kuwa anamdai takribani USD MILION 1 na Uchafu.
Kwa mujibu wa
kumbukumbu za Mkataba, inasemekana kuwa, R. Kelly aliahidi kumlipa McDavid USD
Milion 1.3 ambazo ni sawa na zaidi ya Bilioni 2 za Kitanzania, lakini badala
yake alimlipa USD 300,000 na mpaka hivi sasa wanazungushana kuhusu Kiasi
kilichobaki.
Kutokana na hayo, Ex
Manager huyo ameamua kufungua Mashtaka ya madai dhidi ya Kiwango kilichosalia.
EmoticonEmoticon