SIKU CHACHE ZILIZOKATA, davido
aliweza kutweet kupitia account yake ya Twitter, kuwa Maafisa wa Uhamiaji
Nchini Nigeria, ambao anadai walimuonea na kumnyanyasa katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa MURTALA MOHAMMED, kwa sababu za Kifedha.
Lakini baada tu ya Tweet hiyo
kuzagaa kunako Social Networks, Idara Hiyo ya Uhamiaji Nchi Nigeria, imekanusha
madai hayo hasa ya kifedha, huku wakiweka bayana kila kitu ili kuepusha
Matatizo na Msanii huyo pamoja na wananchi Mbali mbali.
Kwa Mujibu wa taarifa maalumu
iliyotolewa na Afisa Habari wa Idara Hiyo ya Uhamiaji, EMEKA OBUA, inasemekana
kuwa davido alimfuata afisa mmoja katika
Uwanja huo wa Ndege Siku ya safari, kwa Dhumuni la Kusafiri kwenda Nje ya Nchi,
akitumia Passport aliyochukua Nchini marekani, ikiwa na namba 460918874, ambayo
ilikatwa Jijini Georgia, DECEMBER 14 209, na inafanya kazi mpaka December 14
2019.
Afisa huyo alizidi kumiminika kuwa,
baada ya Afisa husika kuipitia Passport hiyo na kubaini ina tatizo, alimuambia
Ukweli Davido kuwa, hawezi Kutoka Nje ya Nchi hiyo kwa sababu Passport hiyo
haikuwa na Visa, hivyo ameona ni bora akuonesha passport aliyokatia Nchini
Nigeria.
Baada ya Davido Kuambiwa hivyo,
inasemekana alimuambia afisa huyo kuwa passport ya Nigeria ameisahau Nyumbani,
jambo ambalo Afisa huyo bado hakukubaliana nalo, na kumuambia aelekee nyumbani
kuifuata Hiyo passport.
Baada ya Kuambiwa Hivyo, Davido kwa
kushirikiana na mabaunsa Wake, walianza kumfokea na Kuanza kuzonga Afisa huyo
wa Uhamiaji na kulalamika kuwa inawezekana Vipi ukamzuia Mtu Kusafiri kisa hana
Passport ya Nchi Hiyo, na Anapassport Nyingine ambayo haina Shida.
Hata hivyo inasemekana Kuwa, baadaye
davido alifuata Taratibu zote, na Kuwakilisha Passport ya Nigeria ambayo ina
namba A02227477
iliyochukuliwa Abuja Mnamo August13,
2010 and na itafanya kazi mpaka August 12, 2015.
Katika kukemea hilo , EMEKA amesema tabia kama za
Davido hazifai hasa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa, na Endapo mtu
anahitaji kutumia Passport za aina hiyo, basi huwa kuna Barua maalum ama
maandishi maalumu ili kufanikisha safari.
EmoticonEmoticon