Unaweza Ukashtushwa na maamuzi ambayo Mashabiki
hawa wa Beyonce walichokifanya, lakini
ukweli utabaki Pale pale…
TTM tumeinyaka kuwa MASHABIKI wawili wa Beyonce wamechukua uamuzi
wa kumfungulia Muimbaji wa kike nchini Marekani, BEYONCE “Mrs Carter”, baada ya
Kujeruhiwa katika Show yake.
SASA Baada ya Kupata info Hizo, TTM tuliingia
kazini na kuweza kusaka chanzo cha hayo
yote na hatimaye kupata Mtonyo kamili wa Ishu Nzima.
Kwa Mujibu wa maelezo kutoka kwa wafungua Mashtaka hayo, RAQUE
CASTELLANOS na GABRIELLA DAVIDSON, inasemekana kuwa walielekea kunako Eneo la
United Center katika Jiji la Chicago Mwezi December Mwaka jana, kwa ajili ya
kufuatilai Show ya Bibie huyo Beyonce, wakiwa na Tiketi zao mapema, na hatimaye
kuwahi kabisa eneo ambalo lipo karibu na STAGE,ili waweze kushuhudia Vizuri
kila kinachoendelea.
Wawili hao waliendelea Kusimulia Kuwa, wakati
wako pale kunako STAGE mapema kabisa, Ghafla Milango ya Mbele Ilifunguliwa kwa
Fujo na kasi ya Ajabu na kundi la watu ambao bila shaka walikuwa ni Mashabiki
wa Beyonce Pia, huku likiwavamia wawili hao mahali walipokuwa.
Aidha Baada ya RAQUE na GABRIELLA kustaajabu
kinachoendelea, Ghafla walijikuta wakisukumwa na kukanyagwa huku na kule, jambo
ambalo liliwaletea majeraha makubwa na hasa Athari ya Kiafya, ikiwemo kupoteza
Fahamu, na Kujeruhiwa Vibaya katika baadhi ya Viungo vya Mwili hasa maeneo ya Mifupa.
Katika Kuhitimisha, Wanawake hao wawili walidai
kuwa, Sababu ya wao kumfungulia mashtaka Beyonce, Ni maandalizi Mabovu ya
Sehemu ambayo Mkali huyo wa DRUNK IN LOVE alitakiwa kupiga Show, huku kukiwa
hakuna Ulinzi wa kutosha na hasa mazingira ya kiusalama kwa Mashabiki wake.
Aidha baada ya Tukio hilo kuwakuta Warembo hao
wawili, hatimaye walikimbizwa katika Hospitali iliyokuwa maeneo hayo kwa ajili
ya matibabu, na wala hawakushuhudia Show ya Beyonce waliyoilipia mapema
kabisaaa, kutokana na Mbwadidi hilo..
EmoticonEmoticon