Infact Ni wengi ambao Tunaamini kabisa kwamba Beyonce
na Ndugu yake KELLY Rowland ambao wote kwa Pamoja ni Ex Members wa Ex Crew ya
DESTINY’S CHILD, hawana maelewano Mazuri Kiasi hicho ingawa Wanapiga Story za
hapa na Pale.
Kitengo Cha Chimbua Chimbu kimrpata mtonyo kuwa
kuna Uwezekano mkubwa wa Beyonce kutokuhudhuria Ndoa ya Kelly, kutoakana na
Mpangilio wa Tukio Zima.
Akitolea maelezo Suala hilo ambalo kuna Baadhi
walitarajia kukutana nalo huku wengine wakiamni huenda Ndugu hao watakuwa
pamoja, Kelly Rowland amesema kuwa, maamuzi aliyoyafanya, hayatahusisha Sababu
za Kutokuelewana na Beyonce, infact Hayo yote ameshayasahau, na hayatilii
maanani.
Kelly ambaye hivi Karibuni atafunga Ndoa na
Mchumba wake TIM WITHERSPOON amedai kuwa wanahitaji Ndoa ambayo itakuwa ya Amani,
katika Siku yenye Amani kabisa.
Hivyo Ndoa Hiyo itashuhudiwa ama itahudhuriwa na
watu wachache sana ambao ni Mama Wa Pande Zte Mbili. Hivyo hawana mpango wa
kuongeza Idadi nyingine ya watu, kwani Suala la Ndoa ni la wawili Binafsi.
Tofauti na hayo, Kelly aliongeza kuwa , Ndoa ni
zawadi kutoka Kwa Mwenyezi mungu, na walengwa huwa ni wawili tu, ambao
wanakubaliana kuishi pamoja katika Shida na Raha, hivyo Yeye na Mumewe
Mtarajiwa wanahitaji kutengeneza historia ambayo Itabaki katika maisha yao
Binafsi pamoja na wazazi wao.
Alipoulizwa kuhusu BLUE IVY kurusha yale maua
wakati wawili hao wanapiga Agano lao, Kelly alicheka, na Kusema kuwa, hilo
swali hawezi kulijibu Muda Huu…
Uhusiano wa Members wote watatu waliokuwa
wakiunda kundi la DESTINY’S CHILD, yaani BEYONCE, KELLY ROWLAND na MICHELLE,
ilivurugika, baada ya Beyonce Kujiondoa katika kundi hilo, na kuanza kufanya
kazi zake Binafsi Chini ya Mumewe JAY Z, kipindi hicho akiwa Ni Mchumba wake
EmoticonEmoticon