Ubabe wa Chameleone umeamsha hasira za kumwaga,
hasa kwa mashabiki mbali mbali ambao walihudhuria katika tamasha la Dr. Josee
Chameleone lililokuwa limeandaliwa huko Nchini Rwanda.
Josee Chameleone ambaye ni moja kati ya wasanii
wakali na wakongwe Nchini Uganda na Afrika mashariki Kiujumla, alitia Ngumu
Kupiga Show katika jiji la Kigali, baada ya kubaini kuwa Vifaa vilivyokuwa
Vimefungwa Kunako Steji Hiyo kwa ajili ya Show yake, Vilikuwa havitoi Sound
Nzuri.
Chameleone aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya
kubaini tatizo hilo ambalo anaamini lingemuangusha sana katika Perfomance yake,
na Lawama kubwa akizipeleka kwa Waandaaji wa tamasha Hilo.
Baada ya kufikia Uamuzi huo, wasanii nyota
Nchini Rwanda pia, nao walishindwa kupanda Stejin kutokana na Hali ilivyokuwa
Mbaya hasa kutoka kwa Nyomi la mashabiki ambao walitia Timu Eneo hilo kumshuhudia
Mkali huyo wa TUBONGE akishusha Mbwadidi la Kiburudani.
Kutokana hasira za mashabiki hao, Wengi
walisikika wakitamka Kuwa wanataka Pesa yao , pamoja na damu ya Chameleone,
hasa kwa kupoteza Muda wao, pamoja na Maandalizi yao ya kuja kumshuhudia akiwa
stejini.
Aidha mpaka hivi sasa, Chameleon ambaye ameanza
Shughuli zake za Muziki kuanzia Miaka ya 1990, hajaomba Msamaha kutokana na
Kitendo hicho ambacho hakika kimewachukiza sana Mashabiki zake Nchini Rwanda
EmoticonEmoticon