TTM Tumenyaka Mtonyo Kuwa RAPPA JAY Z amegoma
kuwa best man wa Swahiba ake wa karibu, KANYE WEST, katika
Ndoa yake na Mchumba wake Kanye West, ambayo inatarajiwa kufungwa hivi karibuni..
Baada ya kupata Mchakato huo, kitengo cha
chimbua kilamua kuzama mitandaoni kusaka Full Details, maana ukizingatia Kanye
na Jay Z ni marafiki wa karibu, wamewahi kufanya kazi ya pamoja katika Albam
yao ya WATCH THE THRONE, pia hawajawahi kugombana.
Baada ya kufuatili kwa ukaribu, TTM tumebaini
kuwa, Chanzo cha Jay Z kugoma kuwa Best man wa kanye West , ni kutokutaka
kuonekana katika TV Show ya akina Kim kardashian inayofahamika kwa jina la
KEEPING UP WITH THE KARDASHIANS.
Aidha taarifa bado zinaeleza Kuwa, JAY Z hapendi
kabisa Kipindi hicho cha Kim kardashian, na wala hayuko tayari kuonekana katika
Kipindi hicho.
Pia inasemekana kuwa, baada ya mazungumzo kadhaa
yaliyofanyika, JIGGA alikubali kuhudhuria katika Sherehe ya Ndoa hiyo, lakini
kwa Sharti la Yeye na familia yake, yaani mkewe Beyonce na Mtoto wao wa miaka
Miwili, BLUE IVY, kutokuchukuliwa Video katika Show ya Kim kardashian.
Katika kuongeza hilo, Beyonce pia alikiri
kutokukipenda kipindi hicho na hayuko tayari kumuona mumewe na binti yake sanjari
nay eye, wakionekana katika Reality Tv Show hiyo.
Kwa upande wao maboss wa ETV ambao ndio
warushaji wa kipindi hicho cha Kim kardashian, wamedai kuwa, watatumia Gharama
yoyote kuhakikisha kipindi Hicho kinarushwa live, huku wakijitahidi kuangalia
watafanya nini ili Jay Z abaki kuwa Bestman wa jay Z
EmoticonEmoticon