KAMA Utakuwa unakumbuka vizuri, Siku kadhaa
Zilizopita TTM tulikupa Mchakato Kuwa RIHANNA anamshtaki MHASIBU WAKE kwa Kumsabababishia
hasara Kipindi hayuko katika Suala Zima la Kiuchumi Miaka Kadhaa iliyopita.
SASA baada ya Kusikilizia kwa Umakini zaidi ili
tufahamu kipi ambacho Kimetokea, FINALLY TTM tumezinyaka Kuwa, The beautiful
Baby wa WE FOUND LOVE, Rihanna, ameshinda Kesi hiyo.
Kwa Mujibu wa Mwanasheria wa Rihanna,
anayefahamika Kwa jina la EDWARD ESTRADA, amesema Kuwa, Mhasibu wake Huyo Peter
Gounis alimshawishi Rihanna kununua Jumba la kifahari lenye Tjhamani ya Dola za
Kimarekani Milioni 7 huko SOUTH CALFONIA, kipindi Hicho akiwa Si sawa kabisa
Kiuchumi mnamo Mwaka 2009.
Tofauti na hilo, akaongeza kuwa, Mhasibu wake
huyo huyo alimshawishi RIRI kununua Nyumba nyingine LOS ANGELS ili kuitumia
kama Njia ya Uwekezaji hasa Kibiashara, lakini Mwisho wa siku mambo hayakuwa
Ndivyo.
Mwanasheria Huyo alizidi kutonya kuwa, Bado
Mhasibu wa RIRI alimshawishi kufanya
marekebisho makubwa yaliyogharimu Dola milioni 2 katika Nyumba hiyo ambayo
haikuwa imara na ilihitaji marekebisho makubwa.
Aidha baada ya Kugundua Hilo, RIRI aliamua
Kumtimua Kazi, na Kumfungulia Shitaka la madai ya Dola Milioni 35 Mwaka 2012.
Aidha baada ya Hukumu Kutoka, Mshtakiwa aliahidi
Kurejesha Dola za Kimarekani Milioni 10, ili kumaliza Madai yake.
EmoticonEmoticon