MSANII Mwenye Heshima Yake Nchini Nigeria 2 FACE
IDIBIA, pamoja na Mkewe ANNIE IDIBIA, Wameamua Kujibu mashambulizi baada ya
Kuchafuliwa na Jarida la ICON WEEKLY, pamoja na Mtandao wa AFRICAN CELEB SPY
Nchini Humo, ambao sasa Unafahamika THE AFRICAN EYE.
Kwa Mujibu wa habari Hiyo, Jarida Hilo la ICON
WEEKLY liliandika Kuwa 2 FACE anatarajia Kupata Mtoto na Mfanya kazi wa Benki
Nchini humo, anayefahamika kwa jina la TENIOLA
Jarida hilo linadaiwa kuandika Taarifa ya Uwongo
zaidi Kuwa TENIOLA ambaye alikuwa ni ACCOUNTANT OFFICER wa 2 FACE IDIBIA kwa
Muda Mrefu sasa, alikuwa na Mahusiano naye , huku Uhusiano huo ukizaa Matunda
ya Kupata Ujauzito kwa mamito Huyo.
KATIKA Kutafuta Data zaidi, KITENGO CHA CHIMBUA
CHIMBUA Kutoka TTM, Kilibaini Mtonyo Mwingine Kuwa, Eti, 2 FACE ambaye ni Baba
wa watoto 7 Hivi sasa, alikuwa akimbembeleza TENIOLA Kutokuhusisha Ujauzito huo
na ndoa yake, na kuacha Kuvujisha Siri Nzima, huku akimshawishi zaidi kwa Kumpa
GARI.
Sasa basi, Wanandoa Hao baada ya Kuinyaka Stori
hiyo ambayo ilihamishwa kama ilivyo na Mtandao huo wa Kijamii wa The African
Eye, waliamua Kuvunja Ukimya na kusema Kuwa, Habari Hizo Si za ukweli na Zina
Nia ya Kuharibu Jina lao na Familia yao Kiujumla, jambo ambalo si Jema hata
kidogo.
Katika Tweets ambazo 2 face aliandika
alidhihirisha Kuwa Upuuzi ulioandikwa na Jarida hilo pamoja na Mtandao huo, ni
UZUSHI wa asilimia 100 bila kupinga kabisa, maana Habari hizo hazina hata
chembe ya UKWELI
CHECK TWEETS ZAO:
EmoticonEmoticon