REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MIMI NA MWANZA: JIONI TULIVU KATIKA JIJI LA MWANZA LEO

10:57:00 AM Add Comment
 TUNARUDI MAKWETU: Wakazi wa Mwanza Wakianza kurejea Makwao kutoka katika Shughuli ama Mihangaiko ya Jumamosi

 UNAFIKA HARAKA; Mwanza Ni raha Jamani. Foleni itatoka Wapi?...Ona Mwenyewe

 WAPENDA SOKA: Wadau wa Soka Jijini Mwanza wakiwa wanafuatilia kwa umakini Mechi ya Mpira wa Miguu kwa wanawake, katika Kiwanja cha Nyamagana

 VIPAJI: Mpira wa Miguu kwa Wanawake nao ulikuwa unaendelea katika Kiwanja cha NYAMAGANA. Vipaji vipo jamani

 USAFIRI MWEUPEEE! : Bara bara hazina hata Foleni. watu tunarudi nyumbani bila hata hofu ya kuchelewa

ZIWA VICTORIA: Utulivu wake unaleta Mvuto kwa wakazi wake na Wageni
PICHA ZOTE NA FRANK JOACHIM

PICHA: MTOTO HUYU HANA HATIA...LAKINI ANACHOFANYIWA NA WAZAZI WAKE, NI UKATILI

10:40:00 AM Add Comment

NIMEUMIZWA: Mtotop Saadah Said (3) akiwa amejeruhiwa Jichona Mama yake wa Kambo


POLE: Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi Shirikishi katika Kata ya Igoma Jijini Mwanza, akiwa na Mtoto Saadah


 MAJERAHA: Majeraha ya Mtoto Saadah katika Upande wa Mgongo wake


WATUHUMIWA: Baba Mzazi wa Mtoto Saadah, Bw. Said (Kushoto) na Mama wa Kambo wa Mtoto huyo ambaye ni Mke wa Bw. Said wakiwa Chini ya Ulinzi (PICHA ZOTE NA SAMWEL CHEMU)

IGOMA,MWANZA.
Licha ya Serikali kuzidi kusistiza Ukatili kwa Watoto Majumbani, Katika Kata ya Igoma, Wilaya ya Ilemela,Jijini Mwanza, Mtoto SAADAH SAID mwenye Umri wa Miaka 3, amekuwa akipigwa Vikali na Wazazi wake hasa Mama yake wa Kambo kwa Madai kuwa anajisaidia haja kubwa ovyo yaani "Anajinyea Ovyo"

Akizungumza kwa aibu Nzito,Mama wa Kambo wa Mtoto sada amedai kuwa, humuadhibu hivyo mtoto huyo Mdogo kabisa,kwa kuwa hufanya tukio hilo mara kwa mara,jambo ambalo yeye amelichukulia kama Ukaidi

Taarifa za kukatiliwa kwa Mtoto huyo,zilitolewa na Wasamaria wema ambao pia ni Majirani wa Familia hiyo katika Mtaa wa Mandela, huku wakisemakuwa, tatizo hilo limekuwa ni Kero nalimekuwa likifanyika Mara kwa Mara dhidi ya Mtoto huyo, likifanywa na Wazazi wote wawili.

Na Smith Swai & Samweli Chemu (99.4 METRO FM)




WATCH: THECAMP MULLAS WANACHAFUA

2:55:00 AM Add Comment

Camp Mulla has released a new song dubbed ‘Chafua’ in collabo rapper Collo and singer Tiri who was rumoured to be the one replacing Miss Karun after her exit from the group.
The crew recently performed in Durban, South Africa at the Grand Finale of the MTV All Stars Africa Tour without Miss Karun and Taio Tripper who Sub-sahara records recently confirmed had also left the group.

KUMRADHI: Sikuwa Hewani kwa Siku kadhaa

7:24:00 AM Add Comment

NDUGU ZANGU:
Namshukuru Mungu kwa kuzidikuwafanya mniamini na kutembelea BLOG yangu kila Siku. Ninawashukuru na Ninyi pia kwa hilokwa Kuonesha Uzalendo wa Dhati katika kutambua Kipaji changu.

Siku kdhaa na kiujumla Ni nyingi, sikuwa Hewani hasa ku-update Taarifa mbali mbali katika Blog yangu.
Kiujumla, sikuwa najisikia Vizuri , lakini nashukuru mwenyezi Mungu nimekuwa Moja kati ya Watu wenye afya Tele tayari kwa kazi rasmi.

Ninawapenda sana, na niawashukuru sana kwa Ushirikiano wenu.




S

BET AWARDS 2013: DRAKE AFUNIKA KWA NOMINATIONS, RADIO NA WEASEL KUIBEBA BENDERA YA AFRIKA MASHARIKI

2:38:00 AM Add Comment






BET Awards ’13 Nominations

Best Female R&B/Pop Artist
Beyoncé
Tamar Braxton
Alicia Keys
Rihanna
Elle Varner


Best Male R&B/Pop Artist
Chris Brown
Bruno Mars
Miguel
Justin Timberlake
Usher


Best Group
Macklemore & Ryan Lewis
Mary Mary
Mindless Behavior
Slaughterhouse
The Throne (Kanye West & Jay-Z)


Best Collaboration 2 Chainz f/ Drake – “No Lie”
A$AP Rocky f/ Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar – “Problems”
French Montana f/ Rick Ross, Drake and Lil Wayne – “Pop That”
Kendrick Lamar f/ Drake – “Poetic Justice”
Justin Timberlake f/ Jay-Z – “Suit & Tie”
Kanye West f/ Big Sean, Pusha T and 2 Chainz – “Mercy”


Best Male Hip Hop Artist
2 Chainz
A$AP Rocky
Drake
Future
Kendrick Lamar


Best Female Hip Hop Artist
Azealia Banks
Eve
Nicki Minaj
Rasheeda
Rye Rye


Video of the Year 2 Chainz f/ Drake – “No Lie”
A$AP Rocky f/ Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar – “Problems”
Drake – “Started From The Bottom”
Drake f/ Lil Wayne – “HYFR
Kendrick Lamar f/ Drake – “Poetic Justice”
Macklemore & Ryan Lewis f/ Wanz – “Thrift Shop”
Miguel – “Adorn”
Rihanna – “Diamonds”
Justin Timberlake f/ Jay-Z – “Suit & Tie”
Kanye West f/ Big Sean, Pusha T and 2 Chainz – “Mercy”


Video Director of the Year
A$AP Rocky & Sam Lecca
Benny Boom
Director X
Dre Films
Hype Williams


Best New Artist
Azealia Banks
Joey Bada$$
Kendrick Lamar
Trinidad Jame$
The Weeknd


Best Gospel Artist
Deitrick Haddon
Lecrae
Tamela Mann
Mary Mary
Marvin Sapp


Best Actress
Angela Bassett
Halle Berry
Taraji P. Henson
Gabrielle Union
Kerry Washington


Best Actor
Don Cheadle
Common
Jamie Foxx
Samuel L. Jackson
Denzel Washington


YoungStars Award
Gabrielle Douglas
Jacob Latimore
Keke Palmer
Jaden Smith
Quvenzhané Wallis


Best Movie
Beasts of the Southern Wild
Django Unchained
Something from Nothing: The Art of Rap
Sparkle
Think Like a Man


Subway Sportswoman of the Year
Gabrielle Douglas
Brittney Griner
Candace Parker
Serena Williams
Venus Williams


Subway Sportsman of the Year
Victor Cruz
Kevin Durant
Robert Griffin III
LeBron James
Ray Lewis


Coca-Cola Viewers Choice Award
A$AP Rocky f/ Drake, 2 Chainz and Kendrick Lamar – “Problems”
Drake – “Started From The Bottom”

Kendrick Lamar – “Swimming Pools (Drank)”
Miguel – “Adorn”
Rihanna – “Diamonds”
Justin Timberlake f/ Jay-Z – “Suit & Tie”


Centric Award
Tamar Braxton – “Love and War”
Fantasia – “Lose To Win”
Miguel – “Adorn”
Nas – “Daughters”
Charlie Wilson – “My Love Is All I Have”


Best International Act: Africa
2Face Idibia (Nigeria)
Toya Delazy (South Africa)
Donald (South Africa)
Ice Prince (Nigeria)
R2Bees (Ghana)
Radio and Weasel (Uganda)

Best International Act: U.K.
Marsha Ambrosius
Estelle
Labrinth
Rita Ora
Emeli Sandé
Wiley



NIPO MWANZA, NYUMBANI NILIKOZALIWA. HII NDIYO LADHA YA JIJI LETU

2:15:00 AM Add Comment
 BISMACK ROCK: Moja kati ya Vivutio Vizuri sana katikati ya JIJI la Mwanza. Mawe haya yabo katika Maji ya Ziwa Victoria

 FISH KEEP LEFT: Usione Umati huo wa Watu umejaa hapo ukadhani kwenye hilo eneo kuna tukio la Hatari. Hapo kuna sanamu ya SAMAKI,ambaye Wakazi wengi wa Mwanza na Hata Wageni, hupenda kupiga Picha mbele ama Pembeni ya Sanamu hiyo ya Samaki

 KAMANGA GARDEN: Hii ni Bustani katika Bara bara ya Kutoka Kamanga kuelekea CAPRIPOINT. Inavutia sana na Inang'aa Muda Wote. Karibu Mwanza

 HALIDONDOKI HILO: Moja kati ya Mawe ya Ajabu yanayopatikana ROCK CITY Mwanza. Unaweza dhania linadondoka lakini hulidondoshi hata kwa Greda

 RAILWAY STATION: Kwa wale tunaotumia Usafiri wa GOGO (Treni) Kutoka, Dar, Dodoma, Shinyanga, na Hata Kwingineko, Hapa ndo Mwisho wa Reli yetu kwa Jiji la Mwanza

 LIKO IMARA HILO: Jiwe ambalo liko karibu na Reli ndani ya Jiji la Mwanza. Mwenyewe unawesza dhania pia kuwa litaidondokea Treni, lakini miaka na Miaka, jiwe hilo halijawahi hata Tikisika

 MAGOROFANI: Hii ndio Magorofani ya Mitaa yetu ya Uswahilini. Nyumba zimejengwa juu kwajuu, na Hasa juu ya Jiwe hili na Lingine kama Unavyoona Mwenyewe

 KIVUKO: Hiki ni Kivuko kilichopo Kamanga Ferry: PANTONZ haziko Da'slaam Peke ake, hadi huku zipo aisee

 MVUTO WA AINA YAKE: Bismarck Rock katika Muonekano wa Karibu.

 KARIBU SATO: Utambulisho wa Kitoweo kikuu cha Jiji la Mwanza na Kanda Ya Ziwa


KISIWA: Hiki Ni Kisiwa cha SAA NANE,ambacho pia Ni Hifadhi ya Wanyama Mbali mbali na Kituo cha Utalii hasa kwa Jiji la Mwanza

KUMBUKUMBU: Hii Ni Kumbu Kumbu ya Kihistoria kwa Jiji la Mwanza.

KARIBU MWANZA: Mandhari Yetu Ni Nzuri Sana.

MBEYA YETU:PICHA ZA AJALI TENA WILAYANI RUGWE MKOANI MBEYA JIONI YA JANA MMOJA AHOFIWA KUFA MAJERUHI MWINGINE APELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA

1:18:00 AM Add Comment




AFYA: MATUMIZI YA SIMU KWA WAUGUZI WAKATI WA KAZI

12:50:00 AM Add Comment



Gordon Kalulunga, Mbeya  
              
WAUGUZI nchini wameshauriwa kuacha simu zao katika vyumba maalumu au kuzizima wakati wanapotoa huduma kwa wagonjwa.

Wito huo ulitolewa juzi na muuguzi mstaafu Andulile Mwansyange (68) alipokuwa akitoa tofauti ya utumishi wake na uuguzi wa sasa katika maadhimisho ya Siku ya Uuguzi Tanzania iliyofanyika Mbalizi-Ifisi, Mbeya.

Mwansyange alisema mjadala unahitajika kuhusu umuhimu wa wauguzi kutotumia simu za viganjani wakiwa kazini.

“Kuwe na mjadala wa wauguzi kutotumia simu wanapokuwa kwenye vyumba vya kutolea huduma muhimu pia wagonjwa wafunge simu wanapoingia kwenye matibabu.
…Unaweza kupigiwa simu ya msiba au kupokea ujumbe wa mtu anayekuhusu hali inayoweza kusababisha kuacha kutoa huduma kwa mgonjwa,’’ alisema muuguzi huyo mstaafu.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya Upendo Sanga, alisema angekuwa mkufunzi wa wauguzi angewafundisha maadili na watakaoshindwa angewafukuza uuguzi.

Akisoma risala kwa niaba ya mkurugenzi huyo aliyekuwa mgeni rasmi, mwanasheria wa wilaya hiyo, Prosper Msivala, alisema suala la matumizi ya simu kwenye maeneo ya kutolea huduma limekatazwa na lipo kisheria hivyo halihitaji mjadala.

Naye Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Mbalizi Ifisi inayomilikiwa na kanisa la Uinjilisti Tanzania, Sikitu Mbilinyi, alisema upendo kwa wagonjwa ni tiba, hivyo umefika wakati kwa kila muuguzi kubadilika.
               

RUSHWA: POLISI 16 MBARONI

12:40:00 AM Add Comment



HATIMAYE Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewatia mbaroni askari 16 wanaohusishwa na tuhuma za uhalifu.

Kutangazwa kwa taarifa hiyo kunakuja siku chache baada ya Tanzania Daima kuandika habari juu ya polisi hao kwa kushirikiana na watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuunda mtandao wa kihalifu.

Taarifa ya kukamatwa kwa askari hao zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Kova alisema askari hao wanatuhumiwa kuunda mtandao wa kukusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa ushuru wa serikali.

Licha ya kuweka wazi idadi hiyo kamanda Kova aligoma kuyataja majina ya wahusika bila kuweka wazi kwa nini ameamua kufanya hivyo.

Kova pia alitumia muda huo kuilaumu Tanzania Daima, kwa kuandika habari za uhalifu huo juzi ikiwa ni baada ya uchunguzi wa zaidi ya wiki moja tangu kukamatwa kwa askari hao.

Alisema kabla ya gazeti hili kuandika habari hizo kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita, jeshi hilo lilikuwa limeshawakamata askari wake wanane kutokana na tukio hilo.


“Si kwa kuwa gazeti moja liliandika na ndiyo tumesukumwa kuwakamata wahalifu hawa; tulianza taratibu hizi mapema na tukawa tunasubiri muda muafaka wa kuweka mambo yote hadharani,” alisema Kova.

Hata hivyo Kova jana alishindwa kuweka wazi yalikopelekwa magari yaliyokamatwa kwenye uhalifu husika.

Wakati akishindwa kutaja kama kuna magari yaliyokamatwa, baadhi ya askri waliozungumza na gazeti hili wameshangazwa na hatua hiyo na kumtaka DCP Kova awe mkweli juu ya sakata hilo.

Askari hao wamehoji hatua ya Kova kuwakamata wenzao walioonekana katika picha za video za mnato na kushindwa kuyakamata magari yaliyokubali kushiriki katika uhalifu huo.

“Mnapaswa kujiuliza kama askari wameshafika 16 halafu hakuna gari hata moja lililokamatwa, hao watakuwa wanapelekwa mahakamani kwa ushahidi wa namna gani na kwa nini hayo magari hayakuweza kuchukuliwa katika hizo picha au ni siasa za mzee wetu zimewafanya mkashindwa kuhoji hilo?” alisema mmoja wa askari.


Mtandao huo unadaiwa kufanya kazi kwa takriban miezi sita kabla ya kujulikana na kuchukuliwa kwa hatua dhidi yao.

Kwa mujibu wa Chanzo cha habari, mbinu inayodaiwa kutumiwa ni kwa askari hao kuwasaidia wafanyabiashara kuingiza bidhaa kupitia bandari bubu ya Mbweni, kisha kuzipakia kwenye magari makubwa kwa ajili ya kutawanya bidhaa hizo katika masoko ya jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya bidhaa zinazodaiwa kuingizwa kwa wingi ni runinga, redio, pasi za umeme na kompyuta mpakato.

MNADA BANNER