Wabunge wametishia kuibandua Tume ya Kuratibu Mishahara ya
watumishi wa umma kutokana na hatua yake ya kupunguza mishahara yao.
Tayari mbunge wa Igembe Kusini Mithika Linturi ametangaza
kuwasilisha ombi kwa spika wa bunge la taifa, kutoa nafasi kwa hoja ya kuitaka
tume hiyo ivunjwe huku akidai kuwa Tume imekwenda kinyume na katiba. Hata
hivyo, Wakili Bobby Mukangi ambaye alihusika katika kuandika katiba anasema
kwamba bunge halina Mamlaka anayodai Linthuri.
Anasema tume ya kuratibu mishara ya watumishi wa umma ni
huru na haiwezi kushinikizwa na yeyote inapotekeleza majukumu yake.
Kwa mujibu wa Katiba tume hiyo ndiyo yenya mamlaka ya
kuratibu mishahara ya watumishi wa umma wakiwemo wabunge.
EmoticonEmoticon