Rais Uhuru Kenyata amepunguza kiwango cha wizara serikalini
kutoka 44 hadi 18.
Kwenye mabadiliko hayo; afisa ya Rais itakuwa na afisi
tendaji ya Rais na afisi tendaji ya Naibu Rais ambapo kutakuwa na wizara mbili
ambazo ni Wizara ya Masuala ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Taifa na Wizara
ya Ugatuzi na Mipango.
Wizara nyingine ni ile ya Ulinzi, Wizara ya Masuala ya Nje,
Wizara ya Elimu, itakayokuwa na idara za elimu na ile ya sayansi na teknolojia,
Wizara ya Taifa ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Uchukuzi na
Miundomisingi,
itakayokuwa na idara za huduma za usafiri na ile ya miundomisingi.
Aidha kuna Wizara ya Mazingira, Maji na Maliasili, Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Miji, Wizara na Habari, Mawasiliano na Teknolojia,
Wizara ya Michezo, Utamaduni na Sanaa, Wizara ya Leba, Huduma za Jamii na
Usalama, Wizara ya Kawi na Masuala ya Mafuta, Wizara ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Wizara ya Biashara na Utalii na Wizara ya Uchimbani
Majini.
EmoticonEmoticon