Idadi ya watu walioaga dunia kwenye shambulizi alhamisi
usiku mjini Garissa imefikia 9, baada ya wengine watatu kufariki wakikimbizwa
hospitalini.
Hii ni baada ya watu wasiojulikana kuvamia hoteli moja mjini
humo wakiwa wamejihami kwa bunduki aina ya AK-47 na kuwamiminia risasi wateja
waliokuwa ndani ya hoteli hiyo kwa jina 'Kwa Chege'. Mkuu wa polisi mkoa wa
kaskazini mashariki Charlton Muriithi amesema kuwa kufikia sasa hawajabaini
lengo la mauaji hayo ambayo yamesababisha taharuki kutanda mjini Garissa.
Ikumbukwe kuwa mapema
mwezi huu mwanafunzi aliuawa huku watu wengine watatu wakijeruhiwa baada ya
watu waliojihami kutekeleza uvamizi katika kioski kimoja mjini humo.
Vile vile, mwanzoni mwa mwezi Aprili, maafisa wawili wa
polisi waliuawa na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Al Shabaab.
EmoticonEmoticon