Harakati na vyama vya siasa katika jimbo la Darfur magharibi
mwa Sudan vimeitaka Sudan Kusini kutowaunga mkono waasi wa jimbo hilo.
Hayo
yameandikwa na mtandao wa Sudan Sifari na kuongeza kuwa, harakati na vyama
kadhaa vya siasa katika jimbo hilo la Darfur ambavyo vilisaini makubaliano ya
amani, leo vimetoa ujumbe wa kuitaka serikali ya Juba kukomesha uungaji mkono
wake kwa makundi ya waasi vikiwemo vyama vya muungano wa mrengo wa mapinduzi
vinavyoendesha shughuli zao nchini Sudan.
Aidha ripoti hiyo imeitaka Sudan
Kusini kuwaondoa ardhi za Sudan waasi wanaobeba silaha sambamba na kusitisha
msaada wake kwa makundi hayo.
Msemaji rasmi wa Muungano wa Harakati na Makundi
ya Siasa katika jimbo la Darfur Hisham Othman Lahu amesema kuwa, kuondolewa
waasi hao ni suala linalopewa kipaumbele zaidi katika fremu ya makubaliano ya
amani.
EmoticonEmoticon