RAis wa Iraq Jalal Talaban |
Rais Jalal Talabani wa Iraq amesema kuwa, utawala wa
Kizayuni wa Israel ndiyo muenezaji wa ugaidi ulimwenguni.
Rais wa Iraq amesema
hayo mjini Baghdad katika mazungumzo yake na Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi,
Waziri wa Ulinzi wa Iran na kusisitiza kwamba, Israel ikiwa na lengo la kulinda
maslahi yake na uwepo wake imekuwa ikieneza ugaidi katika Mashariki ya Kati.
Rais wa Iraq ameashiria uhusiano mkongwe wa Iran na Iraq na kubainisha kwamba,
kiwango cha uhusiano wa nchi mbili hizo ni imara na kisichoweza kutiwa dosari.
Kwa upande wake Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi, Waziri wa Ulinzi wa Iran
amesifu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tehran na Baghdad katika uga wa
kiulinzi.
Waziri wa Ulinzi wa Iran aliwasili jana mjini Baghdad kwa mwaliko wa
Sadun Farhan al-Dulaymi, Waziri wa Ulinzi wa Iraq ambapo akiwa nchini humo
tayari amekutana na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo akiwemo Rais Talabani,
Waziri Mkuu Noury al-Maliki na viongozi wengine wa ngazi za juu wa nchi hiyo.
EmoticonEmoticon