Serikali ya Marekani kwa kupitia Mahakama ya Washington, inakusudia
kuonyesha propaganda zilizo dhidi ya Uislamu katika mitaa na barabara za
Washington, mji mkuu wa nchi hiyo.
Serikali ya Marekani imeeleza kuwa, mpango huo unasubiri hukumu ya mahakama
ya Washington ambayo inatarajiwa kutolewa wiki ijayo. Propaganda hizo ziliwahi
kuonyeshwa na kubandikwa kwenye vituo vya treni ya chini ya ardhi mjini New
York wiki kadhaa zilizopita.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, propaganda hizo ambazo
zimepewa jina la 'Kufeli kwa Jihad' zilisambazwa kwa makusudi mwezi uliopita
mjini New York, na zimepangwa kuonyeshwa tena hivi karibuni mjini Washington
baada ya kupatikana kibali cha mahakama ya jiji hilo.
Takwa la makundi ya
Kiislamu nchini Marekani la kuondoshwa propaganda hizo kwenye vituo vya treni
za chini ya ardhi mjini New York, lilipelekea kuibuka misuguano mikali
kwenye vyombo vya mahakama vya eneo hilo, na kupelekea Jaji wa Mahakama
ya Fideral kueleza kwamba hatua hiyo iko sahihi kutokana na kuwepo sheria
ya uhuru wa kujieleza. Inatarajiwa kuwa, faili hilo litachunguzwa zaidi kwenye
mahakama ya Washington kabla ya kutolewa kibali cha kusambazwa propaganda hizo
zilizo dhidi ya Uislamu.
EmoticonEmoticon