Na Franklin Naceeb-Aboud (Mwana Facebook) & DW
Kiasi ya watu 39 wamekufa nchini Venezuela baada ya mripuko
kutokea katika mojawapo ya viwanda vikubwa vya mafuta nchini humo hapo jana.
Inaaminika kuwa gesi aina ya propane ilivuja na kusababisha mripuko mkubwa
katika kiwanda hicho cha mafuta Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo. Wengi wa
waliokufa ni walinzi wa kitaifa.
Watu
wengine karibu 80 walijeruhiwa katika mkasa huo. Waziri wa
Nishati Rafael Ramirez amesema kumetokea madhara makubwa katika miundi mbinu na pia
katika nyumba zilizokuwa mbele ya
kiwanda hicho. Aliongeza kuwa mripuko huo uliyakumba hadi maeneo yaliyo karibu
na kiwanda hicho.
Lakini hali imerejeshwa kuwa
ya kawaida. Rais Hugo Chavez ametangaza siku tatu za maombolezi akisema
mkasa huo ni msiba kwa familia yote ya Venezuela ikiwa ni pamoja na raia pamoja
na jeshi.
EmoticonEmoticon