Na Frank M. Joachim & DW.
Risala za rambirambi zinaendelea kutolewa kufutia kifo cha
mtu wa kwanza kufika mwezini, mwana anga wa Marekani Neil Armstrong.
Armstrong
aliyekuwa na umri wa miaka 82, alifariki muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji
wa moyo. Alikuwa kamanda wa kikosi cha safari ya Apollo 11 - pamoja na
mwanaanga mwengine Buzz Aldrin.
Mamilioni ya watu duniani kote waliweza
kufuatilia kwenye televisheni mnamo
mwaka wa 1969, jinsi Armstrong alivyotua mwezini, umbali wa kilometa 400,000
kutoka kwenye sayari ya dunia.
Armstrong alisema wakati huo kwamba
alichokifanya, ilikuwa ni hatua fupi kwake kama binadamu mmoja, lakini ilikuwa
ni hatua ndefu mbele, kwa binadamu wote duniani. Rais Barack Obama amemsifu
mwanaanga huyo kuwa ni shujaa mkubwa kabisa wa Marekani ambae kamwe hatasahaulika.
EmoticonEmoticon