Na Frank M. Joachim & DW
Kiasi ya watu 36 wamekufa leo katika ajali mbaya baada ya
lori iliyokuwa imebeba kemikali ya methanol kugongana na basi la abiria la
ghorofa mbili.
Hiyo ndiyo ajali mbaya kabisa ya barabarani kuwahi kutokea China
katika kipindi cha mwaka mmoja. Magari yote mawili yaliwaka moto na ni watu
watatu tu kati ya 39 waliokuwamo ndani ya basi hilo walionusurika kifo katika
ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa nane usiku.
Kwa mujibu wa shirika la habari
la China, Xinhua, jumla ya miili 36 ilichopolewa kutoka kwenye vifusi na watatu
walionusurika wakakimbizwa hospitalini. Mnamo mwezi Julai mwaka jana, moto
ulizuka ndani ya basi moja lililojaa abiria kupita kiasi, na ambalo lilikuwa
limebeba vifaa vinavyoweza kusababisha moto, na kuwaua abiria 41 nchini humo.
EmoticonEmoticon