Gwiji la uigizaji katika tasnia ya filamu Swahiliwood
Hashimu Kambi amejitosa rasmi katika uandaaji wa filamu akiwa mtayarishaji wa
filamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la “Binti Yangu“, filamu hiyo ipo
katika hatua za mwisho kukamilika na kuingia sokoni mwezi huu wa nane. Kwa
mujibu wa Hashimu Kambi kuwa filamu ya
Binti yangu ni kazi yake ya kwanza ambayo ameiandaa na kuwashirikisha wasanii
wakali lengo anataka kuelekea katika kuwa mtayarishaji mkubwa wa filamu za
Swahiliwood.
Hasheem Kambi |
Wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ni Grace Mapunda,
Lucy Komba, Mohamed Funga funga ‘Jengua’, Heriety Chumila, Diana Exavery,
Jennifer Raymond ‘Penina, Jumanne Mshindo, Hashimu Kambi ‘Ramsey’ na wasanii
wengine wakali katika tasnia ya filamu Swahiliwood.
EmoticonEmoticon