Duru za habari kutoka Marekani zimearifu kuwa, mamia ya
wanafunzi wa chuo kikuu cha Mississippi katika jimbo la Mississipi, wamefanya
maandamano makubwa kupinga ushindi wa Rais Barack Obama.
Wanafunzi hao
wanaokadiriwa kufikia 400 walimiminika mabarabarani kupinga hatua ya
kuchaguliwa mara ya pili rais Obama. Chuo kikuu hicho kimetoa ripoti kuwa,
mikusanyiko ya wanafunzi ilianza tangu siku ya Jumanne usiku na kuongezeka
zaidi jana na leo.
Wanafunzi hao waliokuwa wamejawa na hasira walibeba mabango
mbalimbali huku wengine wakitoa nara za kulaani ushindi huo wa Obama. Kufuatia
purukushani hizo, polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi
kuwatawanya wanafunzi hao.
EmoticonEmoticon