PARIS, Ufaransa.
Siku hadi siku idadi ya Wafaransa wanaoishi nchini ya mstari
wa umasikini inazidi kuongezeka.
Televisheni ya France 24 jana ilitangaza
ripoti ya kila mwaka ya taasisi ya misaada ya Kanisa Katoliki kuhusiana
kuendelea kuongezeka kiwango cha umasikini nchini humo.
Ripoti hiyo
iliyotangazwa jana asubuhi inasema kuwa, hivi sasa mwananchi wa Ufaransa badala
ya kutatuliwa matatizo yake ya kiuchumi yanayomkabili, ndio kwanza anazidi
kukabiliwa na matatizo zaidi.
Televisheni ya France 24 imeendelea kusema kuwa,
ukosefu wa ajira na makazi, ni miongoni mwa matatizo makubwa yanayozidisha hali
ya umasikini nchini humo na kwamba, juhudi za kuepukana na hali hiyo zinazidi
kukabiliwa na changamoto nyingi na ngumu.
Idadi ya watu wanaoishi chini ya
kipato cha Euro 680 kwa mwezi inazidi kuongezeka ikilinganisha na miaka miwili
iliyopita nchini Ufaransa. Hivi sasa kiwango hicho kimeongezeka kutoka watu 65
elfu na kufikia watu milioni mbili. Na Sudi Jafar
EmoticonEmoticon