NEW YORK, Marekani.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana lilisisitizia
udharura wa kukomeshwa mara moja mapigano ya watu wenye silaha nchini Libya.
Mjumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Twariq Matri, ambaye
aliwahutubia wajumbe wa Baraza hilo hapo jana kwa kupitia mkanda wa video,
alisema kuwa, viongozi wa Libya wanapaswa kutekeleza marekebisho ya haraka
katika sekta za kiusalama na vyombo vya mahakama kwa ajili ya kuzuia mapigano,
uvunjwaji wa haki za binaadamu, mateso na vitendo vyote vinavyokinzana na
sheria za nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Kuhusiana na uundwaji wa serikali
mpya ya Libya mwezi Julai amesema kuwa, hiyo ni hatua muhimu nchini humo
itakayosaidia kuleta uthabiti na wakati huo huo kumaliza changamoto za
kiusalama na vitendo vinavyokinzana na sheria za taifa hilo.
Aidha mjumbe huyo
wa UN nchini Libya, amezungumzia hatua hafifu zilizochukuliwa na Tripoli kwa
ajili ya kukabiliana na makundi ya wabeba silaha na kusema kuwa, serikali ya
Libya inahitaji kutekeleza marekebisho katika jeshi na taasisi za kiusalama za
nchi hiyo.
EmoticonEmoticon