WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
MPITA NJIA : MH. MAGUFULI, TAFADHARI TUSAIDIE KATIKA HILI...TUNATESEKA !!!!
Haya Ni Maeneo Ya Manzese ambako Ujenzi wa Bara bara ya Mabasi yaendayo kwa Kasi unafanyika Hivi sasa. Lakini Licha ya Ujenzi huo, Kuna kero kama ambavyo unajionea Mwenyewe, hali ambayo ni hatari kabisa kabisa kabisa zaidi ya kabisa, kwa Maisha ya Kila Mtanzania ama Mkazi wa Dar es salaam anayefika Eneo Hilo. Hiovi Ndivyo "MPITA NJIA" nilivyojionea, na nnaomba na wewe Ujionee Pia....hapo ni Foleni ya kwenda Posta, gari zinapita hadi kwenye Ujenzi.
Foleni Kutoka City Center (Posta/ Kariakoo) inakuwa ndio mahala pake kuanzia saa Nane Mchana.
Abiria hawana Sehemu maalumu ya Kusubiri Magari, namaanisha KITUO CHA DALA DALA. Hadi Leo, nimeshuhudia Watu wakiwa Wamesimama Hivi Kimakundi makundi kuanzia Magomeni KAGERA.
Magari Yenyewe hayasimami Abiria Tukapanda. Tunasubiri mpaka Basi...yaani ni Tafrani Tupu, tunaweza tukaibiwa Simu Zetu na Bidhaa zetu hasa Mida ya Jioni kabisa
Vumbi ndio Mahala Pake. Mafua na Magonjwa Mengine ya Kuambukiza kwa Njia ya Hewa hususan Vumbi yanaambukizwa Kirahisi tu....
Haifahamiki Wapi Kwa Watembea kwa Miguu, Watumia Piki Piki na Baiskeli, Magari Makubwa na Madogo Madogo, na Bajaji. Yaani Tafrani Tupu hasa ikiwemo HATARI YA AJALI za Makusudio kabisa.
Hakuna Kituo Maalum Cha Boda Boda, Hali inayohatarisha Maisha Ya Watoto na Wakazi wa Dar
WAPIGA DEBE ndo wasumbufu kupita Maelezo...asipolipwa Hela yake, Gari haliondoki, Hali inayosababisha Foleni kupita Kiasi, Wizi hauishi, magari Tugombanie....ili Mradi Tafrani TUPU
Wapiga Debe wenyewe wamekaa KI-WIZI WIZI.Sasa Kama Huyo(Mwenye Tisheti Nyekundu iliyochanika), anaita abiria?...au anatafuta Kitu kilichokaa Vibaya ili apite nacho?
Magari Yenyewe Tunagombania na Kujazwa kama Matikiti Maji
Wanafunzi ndio Kwanza Masikini ya Mungu hawajui wakimbilie wapi
Haya....Licha ya Vumbi, Uchafu, Mirundikano ya Watu, Mikono Michafu, Biashara ya MACHUNGWA ndio Kwanza inachukua Nafasi. Hii si Hatari kwa Afya Yetu Jamani? (Kwanza Hata Maji ya Kuoshea hayop Machungwa yako Wapi?)

HONGERA ANORD KAYANDA WA CLODS FM
Hivi Ndivyo Anord Kayanda na Mke wake Anitha Ruhinda Kayanda Walivyokula Kiapo Katika Kanisa la MT JOSEPH
Dah.....tushakula Kiapo tayari
Kit cha Keki hichoooooo
Duuuuuh...Cheki Mng'ao huo
Champagne Zilikuwepo kama unavyoona
Wacha weee....wapambe walichangamka Balaa
Mzee Wa Amplifier MILLARD AYO aling'aa Hivi na Mrembo Huyo.
(Picha kwa Hisani ya BAAB KUBWA)
HIVI NDIVYO P. DIDDY ALIVYPOATA AJALI SIKU YA JANA....
Msanii wa Kundi La Dirty Money na Boss Wa BAD BOY ENTERTAINMENT nchini Marekani, Sean Combs P.Didy akiugulia Maumivu baada ya Kupona katika Ajali iliyotkea Jana Mchana
Askari Polisi wakiwa Kwenye eneo la Tukio ambako Didy alipata Ajali
Utaratibu wa Kuliondoa Gari katika Eneo la Tukio Ukifanyika.
P. Didy akionekana Kutembea kwa Kuchechemea.
Akipata Huduma ya Kwanza Mara baada ya Ajali
Gari La P. Diddy lililopata ajali likiwa Nyang'a nyang'a kama unavyoliona
Diddy akijikagu kama namajeraha katika Mkono wake
P. Diddy akiwa na Askari Polisi mara baada ya Kufikishiwa Taarifa
Polisi wakichukua Melezo ya Ajali hiyo
Utaratibu wa Kulichukua gari hilo kutoka katika eneo la Tukio ukiendelea
Didy akiwa Amepata Ahueni baada ya Ajali hiyo
LIBYA HAKUKALIKI
BAN WALID, Libya
Serikali ya Libya imetangaza kuwa makundi ya wapiganaji wanaoiunga mkono
serikali yameudhibiti mji wa magharibi wa Bani Walid uliokuwa ngome ya wafuasi
wa Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Wapiganaji wanauinga mkono
serikali wengi wao wakitoka mji wa Misrata wamekuwa wakikabilina na wafuasi wa
Gaddafi kwa siku kadhaa, mapigano ambayo yamewalazimisha maelfu ya watu
kukimbia mji huo mwezi huu.
Serikali ya Libya imesema mapigano yamesitishwa na
kwamba vikosi jeshi la nchi hiyo vitadhamini usalama wa mji huo na kusimamia
operesheni ya kutoa misaada. Omar Baoughdad kamanda wa wanamgambo wa Misrata
amesema, vikosi vyake vitaendelea kubakia Bani Walid kwa lengo ya kuyafukuza magenge
ya wafuasi wa Gaddafi.
Mji huo uliopo umbali wa kilomita 140 kusini mashariki mwa mji mkuu Tripoli
ulikuwa ngome ya mwisho ya dikteta Muammar Gaddafi aliyepinduliwa na kuuawa
nchini Libya mwaka uliopita.
SUDAN : UN TAFADHARI......
KHARTOUM, SUDAN.
Sudan imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani hatua ya
Israel ya kukiuka ardhi yake na kushambulia kiwanda cha silaha mjini Khartoum.
Waziri wa Habari wa Sudan Ahmed Bilal Osman jana alisema kuwa, ndege nne za
kivita za Israel zilishambulia kiwanda cha Yarmouk Jumanne usiku na kwamba watu
wawili waliuawa.
Daffa-Alla Elhag Ali Osman Mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa
amesema shambulizi hilo ni ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya umoja huo ya
kuimarisha amani na usalama duniani na ametaka hatua hiyo ilaaniwe
kimataifa.
CONFIRMED: H.BABA AMFANYIA KWELI FLORA MVUNGI
H.Baba akimvalisha Pete ya Uchumba Mpenzi wake wa Muda Mrefu Flora Mvungi
H.Baba akipeana Mkono wa Pongezi sambamba na Kusalimiana na Ndugu na Jamaa waliohudhuria katika Tukio hilo Muhimu na la Kipekee
Flora Mvungi kabla ya Kuvalishwa Pete ya Uchumba na H. Baba
Ndugu Jamaa na Marafiki waliohudhuria katika Tukio hilo muhimu
Mkono wa Pongezi na Salam ukiendelea
(Picha zote kwa Hisani ya Mpekuzi)
HAYA HAYA...KWANI ILIKUWAJE?
ULE uchumba uliodumu kwa muda mrefu kati ya mastaa filamu na
muziki wa Bongo Fleva nchini, Hamis Baba ‘H. Baba’ na Flora Mvungi umefikia
pazuri baada ya H – Baba kumtolea mahari na kumvalisha pete ya uchumba.
Tukio hilo lililokuwa na mvuto wa aina yake lilichukua
nafasi siku chache zilizopita, katika Ukumbi wa The Atriums Hotel, Sinza – Afrika Sana,
Dar na kuhudhuriwa na ndugu wa pande zote mbili.
SASA H.BABA SI NDO HUYU ANAFUNGUKA SASA?
“Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikisha tukio
hili, japokuwa gharama ilikuwa kubwa lakini niliweza kujitutumua mwenyewe bila
kuomba mchango kwa mtu yoyote.....Alisema H baba na kuongeza kuwa....
“Jambo kubwa ninalotamani litokee na ninaamini litafanikiwa
ni kufunga ndoa na Flora wangu. Ninampenda sana na nina uhakika na uchaguzi
wangu.”H-BABA
NA MASTAA WALIOHUDHURIA JE?
Baadhi ya mastaa waliohudhuria ni pamoja na Baby Madaha,
Kulwa Kikumba ‘Dude’, Hisani Muya
‘Tino’, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,
Husna Idi ‘Sajenti’ na Wilson Makubi aliye Katibu wa Shirikisho la Filamu
Tanzania (TAFF).
Subscribe to:
Posts (Atom)