KHARTOUM, SUDAN.
Sudan imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani hatua ya
Israel ya kukiuka ardhi yake na kushambulia kiwanda cha silaha mjini Khartoum.
Waziri wa Habari wa Sudan Ahmed Bilal Osman jana alisema kuwa, ndege nne za
kivita za Israel zilishambulia kiwanda cha Yarmouk Jumanne usiku na kwamba watu
wawili waliuawa.
Daffa-Alla Elhag Ali Osman Mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa
amesema shambulizi hilo ni ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya umoja huo ya
kuimarisha amani na usalama duniani na ametaka hatua hiyo ilaaniwe
kimataifa.
EmoticonEmoticon