BAN WALID, Libya
Serikali ya Libya imetangaza kuwa makundi ya wapiganaji wanaoiunga mkono
serikali yameudhibiti mji wa magharibi wa Bani Walid uliokuwa ngome ya wafuasi
wa Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Wapiganaji wanauinga mkono
serikali wengi wao wakitoka mji wa Misrata wamekuwa wakikabilina na wafuasi wa
Gaddafi kwa siku kadhaa, mapigano ambayo yamewalazimisha maelfu ya watu
kukimbia mji huo mwezi huu.
Serikali ya Libya imesema mapigano yamesitishwa na
kwamba vikosi jeshi la nchi hiyo vitadhamini usalama wa mji huo na kusimamia
operesheni ya kutoa misaada. Omar Baoughdad kamanda wa wanamgambo wa Misrata
amesema, vikosi vyake vitaendelea kubakia Bani Walid kwa lengo ya kuyafukuza magenge
ya wafuasi wa Gaddafi.
Mji huo uliopo umbali wa kilomita 140 kusini mashariki mwa mji mkuu Tripoli
ulikuwa ngome ya mwisho ya dikteta Muammar Gaddafi aliyepinduliwa na kuuawa
nchini Libya mwaka uliopita.
EmoticonEmoticon