Foleni Kutoka City Center (Posta/ Kariakoo) inakuwa ndio mahala pake kuanzia saa Nane Mchana.
Abiria hawana Sehemu maalumu ya Kusubiri Magari, namaanisha KITUO CHA DALA DALA. Hadi Leo, nimeshuhudia Watu wakiwa Wamesimama Hivi Kimakundi makundi kuanzia Magomeni KAGERA.
Magari Yenyewe hayasimami Abiria Tukapanda. Tunasubiri mpaka Basi...yaani ni Tafrani Tupu, tunaweza tukaibiwa Simu Zetu na Bidhaa zetu hasa Mida ya Jioni kabisa
Vumbi ndio Mahala Pake. Mafua na Magonjwa Mengine ya Kuambukiza kwa Njia ya Hewa hususan Vumbi yanaambukizwa Kirahisi tu....
Haifahamiki Wapi Kwa Watembea kwa Miguu, Watumia Piki Piki na Baiskeli, Magari Makubwa na Madogo Madogo, na Bajaji. Yaani Tafrani Tupu hasa ikiwemo HATARI YA AJALI za Makusudio kabisa.
Hakuna Kituo Maalum Cha Boda Boda, Hali inayohatarisha Maisha Ya Watoto na Wakazi wa Dar
WAPIGA DEBE ndo wasumbufu kupita Maelezo...asipolipwa Hela yake, Gari haliondoki, Hali inayosababisha Foleni kupita Kiasi, Wizi hauishi, magari Tugombanie....ili Mradi Tafrani TUPU
Wapiga Debe wenyewe wamekaa KI-WIZI WIZI.Sasa Kama Huyo(Mwenye Tisheti Nyekundu iliyochanika), anaita abiria?...au anatafuta Kitu kilichokaa Vibaya ili apite nacho?
Magari Yenyewe Tunagombania na Kujazwa kama Matikiti Maji
Wanafunzi ndio Kwanza Masikini ya Mungu hawajui wakimbilie wapi
Haya....Licha ya Vumbi, Uchafu, Mirundikano ya Watu, Mikono Michafu, Biashara ya MACHUNGWA ndio Kwanza inachukua Nafasi. Hii si Hatari kwa Afya Yetu Jamani? (Kwanza Hata Maji ya Kuoshea hayop Machungwa yako Wapi?)
EmoticonEmoticon