Na Frank M. Joachim
Wahudumu wa ndani ya ndege za kampuni ya Ujerumani ya
Lufthansa katika uwanja wa ndege wa Frankfurt, ulio na shughuli nyingi, leo
wanaendesha mgomo wa kwanza kati ya mingi inayopangwa kufanya kudai
nyongeza ya mishahara.
Mgomo huo ulianza leo saa 11 za asubuhi za hapa
Ujerumani na utaendelea hadi saa saba mchanz. Msemaji wa kampuni ya Lufthansa
amesema misafara 64 imefutwa hadi sasa, hiyo ni karibu asilimia 25 ya huduma
zinazotolewa.
Na Frank Joachim
Mgomo huo umekuja baada ya chama cha wahudumu wa ndani ya ndege,
UFO, kusema kwamba mashauriano juu ya suala la mishahara yameshindwa kufikia
muwafaka.
Chama hicho kinataka mishahara iongezwe kwa asilimia tano, hivyo
kumaliza kipindi cha miaka mitatu mfululizo ambapo wafanya kazi hao
hawajaongezewa mishahara.
EmoticonEmoticon