Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma |
Na Frank M. Joachim
Waendesha mashtaka huko Afrika Kusini wamewashtaki wachimba
migodi 270 kwa kushiriki katika kuuliwa wafanya kazi wenziwao 34 waliokuwa
wanagoma na ambao waliuliwa kwa risasi na polisi wakati wa michafuko iliotokea
katika mgodi wa madini ya Platinum mwanzoni mwa mwezi huu.
Wachimba migodi hao
wameshtakiwa chini ya sheria ambayo haijawahi kutumika tangu siku za utawala wa
kibaguzi wa rangi. Sheria hiyo inataja kwamba ilivokuwa watu hao walikamatwa
katika mwahala hapo, wakiwa na silaha, basi walishiriki katika mauaji
yaliofanywa na polisi.
Serikali imeanzisha uchunguzi juu ya mkasa huo, lakini
hakuna maofisa wa polisi waliokamatwa.
EmoticonEmoticon