Na Frank M. Joachim.
Mtetezi wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha
Republican, Mitt Romney, ameukubali uamuzi wa chama chake wa kumchagua yeye
kushindana na Rais Obama katika uchaguzi wa mwezi Novemba mwaka huu.
Hotuba yake ya kuukubali uteuzi huo katika mkutano mkuu wa chama hicho
huko Tampa, Florida, ilikuwa ni tukio la kwanza rasmi kwa mwanasiasa huyo
kuchomoza katika jukwaa la kitaifa. Alitaja uzoefu wake kama
mfanyabiashara, jambo ambalo amesema linamweka katika hali ilio bora zaidi
kuliko Obama katika suala la kuongeza ajira nchini Marekani.
Alisema hivi
katika mkutano huo wa Florida: "Nitakapochaguliwa kuwa rais wa Marekani,
nitatumia nguvu na moyo wangu wote ili kuirejesha Marekani mahala
ilipokuweko, na kuyanyua macho yetu yaelekee kwenye mustakbali ulio bora."
Kama sehemu ya mpango wake wa vifungu sita, Mitt Romney alisema ataunda nafasi
za kazi milioni 12.
Pia aliufafanua mpango wake wa kuifanya Marekani ijitegmee
katika nishati ifikapo mwaka 2020. Aliahidi pia kuchukuwa msimamo ulio mkali
zaidi kuelekea Iran na Urusi.
EmoticonEmoticon