NA EDWIN MOSHI
MAKETE
MASHIRIKA yanayojihusisha na
utoaji wa elimu na misaada kwa watu wenyemaambukizi ya Virusi vya ukimwi
wilayan Makete Mkoani Njombe yameshauriwa kupeana taarifa wakati wa kutoa
huduma kwa watu wenyemaambukizi ili kuepusha kuwepo na takwimu sisizo sahihi za
idadi ya watu wanao hudumiwa
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
shirika lisilo kuwa la kiserikali la Masupha linalo jishughulisha na masuala ya
utoaji wa huduma ya elimu kwa watu wenye
maambukizi ya virus vya ukimwi Wilayani hapa
Bi,Aida Chengula alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,
Amesema kutokana nakuwepo kwa
mashirika mengi wilayani hapa yanayofanya kazi zinazo endana za kuwasaidia watu
wenye maambukizi kumekuwepo na mkanganyiko katika kutoa takwimu za idadi sahihi
za watu wenye maambukizi kutokana na watu wanaopatiwa huduma mashrika hayo kuwa
ni walewale,huku takwimu ziki onyesha kuwa idadi ya watu wenye maambukizi ni
kubwa.
Kwa upande wa shirika lake Bi
Aida amesema wamekuwa wakiwahamasisha watu wenye maambukizi ya virus vya ukimwi
kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa huduma stahiki ikiwemo kupatiwa
mikopo itakayo wasaidia kuanzisha miradi mbalimbali na pia kwa upande washirika
inawasaidia kupata idadi sahihi ya watu wanao hudumiwa.
Pia amewataka watu wenye maambukizi
kutoa ushirikiano kwa mashirika kwa kutokujiunga katika kikundi zaidi ya kimoja
kwani kwa kufanya hivyo kutiwezesha serikali na wahisani kuweza kujua takwimu
sahihii,
Aidha amesema shirika lake
limeanza mradi wa kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuwapa mikopo na elimu juu
ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi na kwa wale ambao tayari
wanamambukizi kujua namna sahihi ya kujilinda na maambukizi mapya.
Shirika la masupha limekuwa
likijihusisha na utoaji wa elimu ya matumizi ya dawa za kupunguza makali ya
virusi vya ukimwi,upimaji na uuandaji wa lishe kwa watu wenye maambukizi ya
virusi vya ukimwi wilayani hapa tangu mwaka 2005 na kwa sasa lina hudumia watu
wenye maambukizi 1200.
Pia niitaka kujiridhisha kwa
kupata takwimu sahihi za watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi wilayani
hapa lakini jitihada za kumpata mratibu wa ukimwi na mganga mkuu zimeshindikana
kwa kuwa walikuwa katika majukumu mengine.
EmoticonEmoticon