|
Usain Bolt akichuana Vikali kwenye Mbio za Mita 100, katika mashindano ya Olimpiki, huko London mwaka huu |
|
|
|
Usain Bolt Akishangilia Ushindi |
|
Usain Bolt Katika Pouz.. |
Na Frank M. Joachim
London, UINGEREZA
Katika mashindano ya michezo ya Olimpiki, huko London
Uingereza, Usain Bolt wa Jamaica ameshinda mbio za mita 100 za wanaume. Bolt
alikimbia mbio hizo kwa sekunde 9.63 na hivyo kuweka rekodi mpya ya Olimpiki.
Awali Muingereza Andy Murray, alimshinda Roger Federer na kujinyakulia medali
ya dhahabu katika mchezo wa tennis wa waume. Mjerumani Lilli Scharzkopf
ameshinda medali ya fedha katika mashindano ya michezo saba mbalimbali,
heptathlon. Na muogeleaji Michael Phelps wa Marekani amefunga kazi katika
mashindano ya Olimpiki kwa kushinda medali ya dhahabu katika mashindano ya
kuogelea ya mita 100 kupokezana mara nne. Kwa jumla Phelps ameshinda medali 22
za Olimpiki, 18 kati yake zikiwa za dhahabu.
Share this
EmoticonEmoticon