REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

"Tizameni Matiti Yangu"- KIM KARDASHIAN

11:33:00 AM Add Comment







Na Frank M Joachim

Kim Kardashian alikuwa na Ujumbe Muhimu sana kwa marafiki zake wa Facebook na Tweeter, ambao ni
"Tizama Matiti yangu", huku akiuza sehemu ya nyonyo hizo katika Picha.
Mrembo huyo ambaye amewahi kukumbwa na Skendo la Kupiga Video ya utupu na aliyekuwa mpenzi wake, Ray J, amepachika ama Kupost baadhi ya Picha zake akionesha sehemu za Nido zake, katika ukurasa wake wa facebook na Tweeter kama unavyoona hapo.

 Hali hii inatokana na Mrembo huyo mabaye hivi sasa ni mpenzi wake Kanye West amefanya hivyo ikiwa ni vugu vugu la Mastaa wengi wa Nje hasa wa Kike kuopnesha walivyojipanga katika Msimu wa Majira ya Joto





BIKINI YA BRINEY SPEARS YAFUNIKA...HII HAPA IONE MWEEEENYEWEEEE

11:24:00 AM Add Comment





Na Frank M Joachim

Kudhihirisha kwamba hatamani Kipindi / Majira ya joto yaishe, Mkali wa Pop Britney Spears ameonesha rasmi BIKINI yake ambayo atitumia kunako Summer time
Bikini hiyo imetupiwa kunako TWEETER na FACEBOOK, ambako imepata Followers zaidi ya 19,900,000
"nafurahi sana, sitaki summer hii kuisha"...alipost bibie Huyo

Wafanyakazi wa Ndege wagoma

11:14:00 AM Add Comment











Na Frank M. Joachim

Wahudumu wa ndani ya ndege za kampuni ya Ujerumani ya Lufthansa katika uwanja wa ndege wa Frankfurt, ulio na shughuli nyingi, leo wanaendesha mgomo wa kwanza kati ya  mingi inayopangwa kufanya kudai nyongeza ya mishahara.

 Mgomo huo ulianza leo saa 11  za asubuhi za hapa Ujerumani na utaendelea hadi saa saba mchanz. Msemaji wa kampuni ya Lufthansa amesema misafara 64 imefutwa hadi sasa, hiyo ni karibu asilimia 25 ya huduma zinazotolewa.


Na Frank Joachim
Mgomo huo umekuja baada ya chama cha wahudumu wa ndani ya ndege, UFO, kusema kwamba  mashauriano juu ya suala la mishahara yameshindwa kufikia muwafaka.

 Chama hicho kinataka mishahara iongezwe kwa asilimia tano, hivyo kumaliza kipindi cha miaka mitatu mfululizo ambapo wafanya kazi hao hawajaongezewa mishahara.

SALVY MANYIKA HUYU HAPA TENA....Safari hii....Mjipaaaaaaange

11:14:00 AM Add Comment




Na Frank M. Joachim

Mkali aliyesikisa (Aliyeunguza) vikali kwa kukonga haswaa nyonyo za Mashabiki wa Muziki wa Bongo Flava kupitia Track yake Mpya ya "ZASIKISA" amepania kufunika zaidi katika Track yake Mpya itakayokuja hivi karibuni

Akizungumza na joachimjunior.blogspot.com mapema Leo hii kwa njia ya Simu, Salvy amesema kuwa Track hiyo itakayokwenda kwa Jina la WANANUNA na imepikwa na Untouchable Young Producer D TOUCHEZ anayekuja kuharibu vibaya sana Soko la akina Manecky, Marco Chali, Panco Latino na wengineo kibao ambao wanatishia amani Music Industry hapa Bongo

"Ngoma itakuwa Kali kuliko Zote ambazo nimewahi kufanya, na nimefanyia katika Studio za TOPITO RECORDS zilizoko sumbawanga. Off Course ni Studi changa sana ila ni balaa, coz hata vifaa haijajitosheleza, na ndio maana tunaifanyia maboresho hapa Dar"..alisema Salvy

Aidha katika Upande wa Vide, Manyika ameongeza kuwa itakuwa tayari Muda si Murefu.
Cheki  Mzigo ulivyoandaliwa.
Salvy Manyika Katika Pouz
Hivi ndivyo Vifaa vya Topito Record ya D Touchez..Msigune Mwanzo Mgumu Jamani..Mweeh!
Producer na Mmlikiwa wa TOPITO RECORDS, D Touchez katika BIG POUUUUZ. Huyu ndiye anayepika ngoma ya WANANUNA ya Salvy


Salvy, karibu Studio hapa (TOPITO RECORDS). Kushoto ni D. Touchez na Salvy Manyika (Kulia)


Usalama wa Vifaa. Mic ya Kuingizia Vocal ndani ya Topito records ikiwa Imehifadhiwa na kufunikwa vizuuuuuuuuri...issingiliwe na Vumbi meeeen


"Yeeeah...Yeeeah...Yeeeah.....Zima AC...sikusikii fresh D Touchez". Salvy akiingiza Vocal la ngoma Mpya.




WACHIMBA MIGODI WASHITAKIWA SOUTH AFRICA

10:51:00 AM Add Comment



Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Na Frank M. Joachim

Waendesha mashtaka huko Afrika Kusini wamewashtaki wachimba migodi 270 kwa kushiriki katika kuuliwa wafanya kazi wenziwao 34 waliokuwa wanagoma na ambao waliuliwa kwa risasi na polisi wakati wa michafuko iliotokea katika mgodi wa madini ya Platinum mwanzoni mwa mwezi huu. 




Wachimba migodi hao wameshtakiwa chini ya sheria ambayo haijawahi kutumika tangu siku za utawala wa kibaguzi wa rangi. Sheria hiyo  inataja kwamba ilivokuwa watu hao walikamatwa katika mwahala hapo, wakiwa na silaha, basi walishiriki katika mauaji yaliofanywa na polisi.

 Serikali imeanzisha uchunguzi juu ya mkasa huo, lakini hakuna maofisa wa polisi waliokamatwa.

HATIMAYE ROOMNEY AKUBALI KUVAANA NA OBAMA

10:36:00 AM Add Comment







Na Frank M. Joachim.

Mtetezi wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, Mitt Romney, ameukubali uamuzi wa chama chake wa kumchagua yeye kushindana na Rais Obama katika uchaguzi wa  mwezi Novemba mwaka huu. 

Hotuba yake ya kuukubali uteuzi huo katika mkutano mkuu  wa chama hicho huko Tampa, Florida, ilikuwa ni tukio la kwanza rasmi kwa mwanasiasa huyo kuchomoza katika jukwaa la kitaifa.  Alitaja uzoefu wake kama mfanyabiashara, jambo ambalo amesema linamweka katika hali ilio bora zaidi kuliko Obama katika suala la kuongeza ajira nchini Marekani.

 Alisema hivi katika mkutano huo wa Florida: "Nitakapochaguliwa kuwa rais wa Marekani, nitatumia nguvu na moyo wangu wote  ili kuirejesha Marekani  mahala ilipokuweko, na kuyanyua macho yetu yaelekee kwenye mustakbali ulio bora." Kama sehemu ya mpango wake wa vifungu sita, Mitt Romney alisema ataunda nafasi za kazi milioni 12.

 Pia aliufafanua mpango wake wa kuifanya Marekani ijitegmee katika nishati ifikapo mwaka 2020. Aliahidi pia kuchukuwa msimamo ulio mkali zaidi kuelekea Iran na Urusi.

MNADA BANNER