Ubalozi wa Venezuela Nchini Kenya (Picha na REUTERS) |
Na Frank M. Joachim
Polisi wa Kenya wanasema kuwa
wanaendelea na uchunguzi, juu ya mauaji ya balozi mpya wa Venezuela
nchini humo, ambaye aliuwawa Ijumaa.
Watu hao sita wamekamatwa siku mbili tu baada ya balozi huyo kupatikana amefariki nyumbani kwake.
Siku ya Ijumaa, polisi walisema kuwa maiti ya Bi Olga Fonseca ilipatikana kitandani mwake lakini sababu za kuuwawa kwake hadi sasa hazijulikani.
Bila ya kutoa maelezo zaidi, polisi wamesema kuwa wanawashikilia watu sita kuhusiana na kifo cha balozi huyo.
Taarifa kutoka wizara ya maswala ya njee ya Kenya imesema kuwa wafanyikazi katika makaazi ya balozi huyo waliwasilisha malalamiko yao kwa polisi baada ya kufutwa kazi hivi majuzi.
Inadaiwa kuwa bi Fonseca aliwafuta kazi baada ya wao kukataa kuondoa malalamiko kuhusu madai ya kunyanyaswa kijinisia na mtangulizi wa balozi huo.
Hata hivyo polisi wamesema wanachunguza madai hayo
EmoticonEmoticon