Na Hezron Munisi- UGANDA
HAKUNA kitu kinauma kama pale ambapo mtu anaamua kutumia kipindi kigumu ulichopo kwa ajili ya kutengeneza pesa ama kutengeneza jina lake, ama kutafuta Sifa hasa kwa watu mbali mbali
Na kinachokera zaidi, ni pale ambapo anatumia maneno makali na ushahidi usio na tija ili aendelee kuwaaminisha watu na aendelee kukukandamiza ili aingize mpunga zaidi kwake
Moja kati Ya Blog Nchini Uganda (jina tunalihifadhi) imejikuta akimuudhi na kumkwaza LILIAN MBABAZI mzazi mwenzake na Marehemu Radio kwa kumuandama na kitu ambacho hakina ukweli hasa katika kipindi hiki ambacho bado anaugulia maumivu ya Msiba wa Mzazi mwenzake.
Blogger anayetumia jina la Scoop alipost Picha inayomuonesha Lilian Mbabazi akipiga Kinywaji na Marafiki zake, na kisha kukoment kuwa imekuwa ni mapema sana kwa Bibie huyu kula bata mapema
Tunamnukuu
"Lilian Mbabazi, Mjane wa Mowzey Radio akiwa Out anapiga kinywaji na KARITAS KIRISIMBI na Marafiki wengine. Sio mapema kwake kutoka out na kula Bata, au ni muda wa kusonga mbele?"
Lilian aliscreen Shot Comment hiyo kisha akaandika
"Ka Jambo Scoop, kuchukua picha za Tangu Mwaka 2016 na kuzipost Sasa Hivi... MUSWADDE NYO"
EmoticonEmoticon