Na Baba Juti
#WatuWaMungu Hata kama haijawahi kukutokea, lakini siku
ikifika basi lazima ka hali haka hata kwa Uchache katakukuta Tu automatically
Taarifa za Uhakika zinadai kuwa, NICKI MINAJ huwa anakosa
amani kabisa anaposikia kuwa Rapper Meek Mill yupo karibu ama katika mazingira
ambayo yeye yupo
Hiyo imetolewa na moja kati ya Wapambe ambao huongozana na
Hit Maker huyo wa HIGH SCHOOL wakidai kuwa, hii siyo Mara ya Kwanza Nicki
anaonesha dalili ya kutokuwa na amani hasa pale ambapo Meek Mill anakuwa katika
mazingira ya karibu naye.
Mpambe huyo aliongeza kuwa, Kitendo cha Meek Mill kuingia
katika Club ambayo Nick Minaj alikuwemo kwa ajili ya Party yake, kilimkosesha Raha sana na
kumuacha akiwa mwingi wa wasi wasi katika eneo alilokuwa ameketi.
Tofauti na Umbali ambao wawili hao walikuwa, Inasemekana
NICKI alisisitiza Ulinzi wa Kutosha na wenye Nguvu katika eneo lake, ili
kuepukana na Majanga ambayo yangeweza kutokea Muda wowote
Pia Inasemekana kuwa, Ilifikia Muda Nicki Minaj alizuia Watu
waliokuwa katika Eneo la Meek Mill, kusogea katika Eneo lake, na hata kama
kulikuwa na watu ambao wanapiga Picha, basi alikuwa akijitahidi kuwaminya
EmoticonEmoticon