By
Tausi Ally, Mwananchi-Dar
es Salaam.
Jana, mfanyabiashara Christon Mbalamula (28), alifikishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na shtaka la kutumia mtandao wa Whatsapp kwa kulidhalilisha jeshi hilo.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Dk Yohana Yongolo, Wakili wa Serikali Winifrida Sumawe alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 26, 2016 eneo la Kigamboni.
Alidai siku ya tukio, mshtakiwa huyo alilidhalilisha Jeshi la Polisi baada ya kusambaza ujumbe uliosema,
“Natangaza ndoa na askari yeyote atakayejipendekeza kwangu siku hiyo ataolewa bila mahari.”
Baada ya kusomewa shtaka hilo alikana na upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi haujakamilika.
Hakimu alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na kila mmoja asaini bondi ya Sh1 milioni na kati ya wadhamini hao mmjoa awe na mali isiyohamishika.
Share this
Related Posts
QUEEN DARLEEN-"MIMI NI MWANAMKE, NINA HISIA PIA" Na Hezron Munisi #WatuWaMungu tunaamini kabisa wengi hamjapata kumsikia Queen Darleen akizungumzia Mahusiano
REDSAN KAFANYA FUJO...TAARIFA HII HAPA Na Baba Juti MAPEMA asubuhi ya leo, taarifa zimefikishwa katika dawati la "Hit Zone" kuhus kitendo cha Producer SAPP
2 CHAINZ: MIE NI MTU MZIMA/ MSINIKAGUE KIJINGA. Na Hezron Munis RAPPER 2 CHAINS hakufurahishwa na Ukaguzi aliofanyiwa alipokuwa Airport Nchini Du
MAMBO YAMEKUWA MABAYA : RAPPER T.I ANAOMBA KESI YAKE NA KAMPUNI YA INAYOMDAI...ITUPILIWE MBALI !!!! Na Rich Sam #WatuWaMungu Rapper T.I ameamua kupinga mashtaka ya kukatisha mkataba na kutokulipia "vito"
EmoticonEmoticon