LEO ilikuwa Ni Guud day Kwa MKUBWA HAMIDU ambaye
ameweza Kutambulisha Track yake kupitia Kituo Cha Redio Cha Metro Fm 99.4 Mhz –Mwanza,
katika Kipindi cha Jam Session.
Track hiyo ambayo Inafahamika Kwa jina la NDOTO
ZA MKEO, ina mahadhi Fulani hivi ya Kizazi kipya, huku Mkubwa hamidu akisimulia
Stori ya Aina yake na Ya kibunifu kabisa, kwa Mtindo wa Rap.
Katika Interview ambayo ameifanya kunako kipindi
hicho cha JAM SESSION ambacho huruka kila Jumatatu Mpaka ijumaa, kuanzia 7:00
Mchana mpaka 10:00, HAMIDU amesema kuwa Track yake iko tofauti na Nyimbo ambazo
Zinafanya Vema Hivi sasa katika Soko la Muziki
Nchi, lakini bado anaamini
itafanya Vizuri sana na hata Kuliko hizo.
“Nyimbo yangu Ni kali, wala Sitishiki na Nyimbo
za Kibiashara Kwa hivi sasa. Story yangu inakushawishi Utamani kusikiliza Verse
ya pili mpaka ya tatu.”
Tofauti na hayo, Hamidu amesema kuwa kitu
ambacho kinapatikana Kunako Track hiyo, kinazungumzia Athari za watu hasa
katika jamii Yetu Kukurupuka katika Maamuzi.
“Ninashukuru sana Track yangu inaeleweka, na
Inastory Nzuri. Mpaka hivi sasa, kunako mtandao wa Hulkshare, Ngoma hiyo
imesikilizwa na watu zaidi ya 900, huku ikiwa Downloaded na watu zaidi ya 500. Hivyo
ni hatua Nzuri Kwangu nab ado inazidi kunihamasisha kuwa itakuwa zaidi ya hapo.”
Alisema Mkubwa Hamidu.
Katika kuongezea, Mkubwa Hamidu amesema Kuwa,
Ngoma Hiyo imetengenezwa ROCK TOWN RECORDS iliyoko Mwanza, na Producer ni Yeye
Mwenyewe
EmoticonEmoticon