REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MWANZA : KIWANDA CHA DWA ZA BINADAMU

6:25:00 AM

Kauli hiyo ameitoa Jiji Mwanza wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince phamaceutical cha jijini hapa kilichopo katika Wilaya ya Nyamagana.

Ndikilo amesema haiwezekani hata ajira kama za kukata majani badala yakuwapa wananchi wanaozunguka maeneo haya mkaenda kutafuta mtu kutoka mbali, kwani kwa kufanya hivyo mtawafanya wananchi hawa wasiwe rafiki wa kiwanda na wakati mwingine wanaweza kufanya uhujumu.

Katika hatua nyingine Ndikilo amewaomba mamlaka ya Chakula na dawa nchini kuona uwezekano wa kukifanyia ukaguzi ili waweze  kukifungua kiwanda hicho mapema na  shughuli za uzalishaji ziweze kuanza mara moja.

 " Ndugu zangu haiwezekani kila kitu kimekamilika halafu  wenzetu wa TFDA wanasema watakuja kufanya ukaguzi tarehe ishirini na nane, alisema Ndikilo na kuongeza, lazima wafahamu kuanza kwa kiwanda ni ajira, uzalishaji, ukuzaji wa uchumi n.k" 

Huku akimtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa kanda ya Ziwa kuwasiliana na makao makuu kuona uwezekano wa kufanya ukaguzi wa haraka na kukiruhusu kiwanda hicho kufanya kazi.



Aidha Mkuu huyo wa mkoa, alionya juu ya utunzaji wa mazingira, ulinzi 
wa kiwanda kwa wananchi wanaozunguka na kuhakikisha wakti wote wanatoa ushirikiano kwa Mwekezaji.

Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho Prince Hetal Vithlani, ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wilaya kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipokuwa na dhamira ya kuanzisha kiwanda hicho hapa mkoani,


Katika kuhakikisha anaunga mkono juhudi za Serikali  kuwaletea maendeleo wananchi, Mmiliki wa Kiwanda hicho bw. ametoa Jumla ya Mifuko ya Sementi 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari za Lwanyuma na Buhongwa, zilizopo wilayani Nyamagana sehemu ambayo kiwanda hicho kipo.

Prince Phamaceutical ndicho kiwanda cha kwanza na cha kipekee katika kanda ya Ziwa, ambacho mara baada yakuanza kazi, kitakuwa Tegemeo kwa wananchi wa kanda ya ziwa na Mikoa ya Jirani na kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Nchi Jirani.

CREDIT: G-SENGO


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER