FAHARI NEWS: Mbeya
Watu37 wamejeruhiwa
mara baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka mkoani Mbeya kwenda Dar es salaam
kupasuka tairi na kupinduka katika eneo la Meta, Chimala, Mbarali mbeya.
Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Happy Nation lenye namba
za usajili T. 281 ARR Scania lililokuwa likendeshwa na dereva aliyefamika kwa
jina moja la Shabani.
Taarifa iliyothibitishwa na Kamanda
wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi inasema kuwa basi hilo lilikuwa likitokea
mkoani Mbeya kuelekea mkoani Dar es Salaam.
Amesema ajali hiyo imetokea leo Nov 7 majira ya asubuhi baada ya kupasuka tairi la
mbele kushoto hali ambayo ilisababisha
kuacha njia na kupinduka.
Amesema mara baada ya kupasuka tairi dereva alishindwa kuimudu nahasa
kutokana na eneo lenyewe kuwa na kona kali hivyo aliamua kuligongesha kwenye
ukingo wa barabara nakusabisha hali hiyo.
Aidha Msangi amesema kuwa kati ya
majeruhi hao 29 ni wanaume na wengine 8
nakwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
Amesema kuwa majuruhi
Sita kati ya wote hali zao ni mbaya na tayari wamefikishwa katika
hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi wakati majeruhi wengine 10 wakiwa
wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya Chimala.
Akithibitisha kupokea kkwa majeruhi
hao Muuguzi katika chumba cha msaada wa haraka hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt
Orivia Masoi amesema kuwa wamepokea majeruhi sita ambapo wanne wamelazwa wodini na wawili tayari wameruhusiwa.
Aidha mmoja wa majeruhi Nicolaus Fungo ambaye amelelazwa wodi namba moja kwa ajili
ya matibu hao amesema majeraha makubwa maeneo ya mbavuni na kwamba hali yake
inaendelea vizuri mara baada ya kuaptiwa matibabu.
EmoticonEmoticon