MWANZA, Tanzania
Zawadi
za washindi wa mbio za Rock City zitakazofanyika katika mkoa wa Mwanza tarehe
26 mwezi huu zimetangazwa jana huku mdhamini mkuu wa mbio hizo, Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) likitoa shilingi milioni 15 kuboresha mbio
hizo.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi milioni 15 kwa waratibu wa mbio
hizo, Capital Plus International Limited, Afisa uhusiano wa NSSF, Bw. Jumanne
Mbepo amesema kuwa NSSF imeendelea kudhamini mbio hizi kwa mwaka wa sita
mfululizo kutokana na kuona maboresho yanayofanyika katika mbio hizo kila
mwaka.
“Mbio
hizi zitaambatana na kutoa elimu kwa wakulima na wachimbaji wadogowadogo wa
madini katika kanda ya ziwa, juu ya umuhimu wa kujiunga na mfuko wa NSSF ili
waweze kunufaika na huduma zitolewazo na shirika kama vile mkopo, bima ya afya
pamoja na mafao mbalimbali,” Alisema Bw. Mbepo.
Mratibu
wa mbio hizo, Bw. Matthew Kasonta amesema kuwa udhamini huo utasaidia kwa kiasi
kikubwa kufanikisha maandalizi ya mbio hizo na kuleta maboresho makubwa katika
mbio za mwaka huu. Amesema kuwa maboresho hayo ni pamoja na kuwepo kwa mbio
fupi zitakazo jumuisha vijana kutoka katika shule za sekondari na wale waliopo
shule za msingi madarasa ya juu.
“Baada
ya kupata udhamini huu, tunafaraja ya kutaja zawadi watakazopatiwa washindi.
Kwa mbio za Kilomita 21, jumla ya shilingi milioni saba na laki moja zimetengwa
kwa ajili ya washindi. Washindi wa kwanza watazawadiwa Tsh 1.5m/- huku washindi
wa pili watapata laki tisa na washindi wa tatu watapata laki saba kila mmoja.
Kwa
mbio za kilomita tano, zaidi ya shilingi laki nne zimetengwa kwa ajili ya
washindi. Jumla ya shilingi laki tatu na arobaini zimetengwa kwa ajili ya
washindi wa mbio za kilomita 3 na shilingi laki mbili imetengwa kama zawadi kwa
ajili ya mbio za watoto za kilomita mbili.”
Bw.
Kasonta amesema kuwa kwa mbio fupi ambazo zimeanzishwa mwaka huu (mita 100,
mita 400 na mita 1,500) jumla ya shilingi laki nne na themanini pesa taslimu
zimetengwa kwa ajili ya washindi huku washindi wote wa kwanza (wa kike na
kiume) watapata king’amuzi cha Continental Decoders.
Bw.
Kasonta aliwataja wadhamini waliofanyikisha mbio hizo kuwa ni Shirika la Taifa
la Hifadhi ya Jamii (NSSF), TSN Group kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy,
pamoja na African Barrick Gold, IPTL, Air Tanzania, New Mwanza Hotel, Nyanza
Bottling, Sahara Media Group, Continental decoders, New Africa Hotel, PPF,
Tanapa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
“Nawasihi
watu waendelee kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za usajili katika ofisi za
kampuni ya Capital Plus International Limited (CPI) jengo la ATC ghorofa ya
tatu jijini Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza, Ofisi
zote za wilaya za Michezo na Utamaduni mkoani Mwanza na Uwanja wa Nyamagana,”
alisema Bw. Kasonta.
EmoticonEmoticon