Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents
(TMT) limefikia hatua ya Mwisho kabisa mara baada ya washiriki kumi bora
kupatikana katika Show ya Mchujo iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya
Taifa siku ya Alhamisi.
Show hiyo ya Mwisho katika katika Hatua ya
mchujo ilifanyika siku ya Alhamisi na kupelekea Washiriki watatu kutoka Kanda
Mbili za Tanzania yaani Kanda ya Kati na Kanda ya Pwani kuondolewa katika
Kinyanganyiro hiko na Kupelekea Shindano hilo kubaki na washiriki 10 tu ambao
wameingia hatua ya fainali ambapo mshindi mmoja ataondoka na kitita cha
Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika Fainali Kubwa inayotarajiwa kufanyika
katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya Tarehe 30 Mwezi huu wa Nane.
Washiriki waliondolewa katika Kinyanganyiro Hiko
ni Mwinshehe Mohamed ambae alikuwa mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda
ya Kati ambapo anafanya Idadi ya washiriki wawili kutoka Kanda ya Kati
kuondolewa na Kuifanya Kanda ya Kati kuwakilishwa na Mshindi Mmoja katika
Fainali hiyo. Wengine waliotoka ni Shiraz Ngassa na Fredy Kiluswa ambao wote ni
Washindi kutoka kanda ya Pwani Mkoa wa Dar Es Salaam.
Kanda ya Pwani walichukuliwa washindi watano
huku Shiraz na Fredy wakitimiza idadi ya Washiriki wanne kuondolewa katika
kinyanganyiro hiko kwa Kanda ya Pwani, Tishi Abdallah ndie Mshindi mmoja kati
ya washindi watano kutoka kanda ya Pwani ambae anaiwakilisha Kanda ya Pwani
katika Fainali kubwa ya Shindao la Kwanza na la Kipekee kufanyika Afrika
Mashariki na Kati la Tanzania Movie Talents (TMT).
Mpaka Sasa Ni Kanda Moja tu ambayo washindi wake
wote watatu ndio wanaiwakilisha Kanda hiyo katika Fainali kubwa itakayofanyika
Mwishoni Mwa Mwezi wa Nane katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo mshindi mmoja
ataondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania huku washindi wote
kumi waliofanikiwa kuingia Katika hatua ya Fainali watakuwa chini ya Kampuni ya
Proin Promotions limited ambapo watacheza filamu ya pamoja na Hatimaye kuanza
kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo inayotarajiwa kutoka Hivi Karibu.
EmoticonEmoticon