PANCHO LATINO: Producer Kutoka B-HITZ |
DAR ES SALAAM, Tanzania
THANKS kwa akina dada Wote walioko
katika Music Industry hapa Bongo, ambao pia wana uwezo mzuri wa Kufanya kazi
zao, na sauti zao zikadhihirika kabisa kuwa ziko so Hot, na zimekaa Vyema.
Mfano wa wengi ambao tunajivunia
kuwa na Classic Voice kwa Upande wa Divas, Ni pamoja na Linah Sanga, Ray C,
Linnah Sanga, Lady Jay Dee, Rachel na Wengineo kibao ambao mpaka hivi sasa wako
Vizuri katika game.
LAKINI Siku ya Jana, Pancho Latino
Kutoka B-HITZ, ametishia amani ya Soko la Muziki hasa ule laini kwa Upande wa watoto
wa Kike, baada ya Kutuonjesha Sauti na Mzigo Mpya ambao Soon utaanza kukita Air waves hapa Bongo na
hata kimataifa
Katika Kauli yake PANCHO,
alidhihirisha kuwa, Ni Kipaji cha Ajabu kutoka kwa Binti huyo, anayetumia Jina
la Rosemalley
Ingawa bado mzigo haujafahamika ni
Mkwaju gani na Utatoka lini, lakini kwa masikio ya TTM, imedhihirika kabisa
Bibie huyu atakuja kuhatarisha Sokola Muziki wa Kizazi Kipya hasa kwa
Malegendary na wale ambao tayari wameshatangulia katika Soko la Muziki.
EmoticonEmoticon