SIKU ya jana TTM tulikupa Full
mtonyo kuhusu Ishu ya Dully Sykes kufungukiwa kuwa anapenda Kuhongwa, na Yuko
katika mahaba mazito na Bibie mmoja anayefahamika kwa jina la BWEDAHA MALANGA…
SASA, Baada ya Kukaa macho
kufuatilia kwa umakini mchakato mzima unavyoenda, hatimaye kupitia account ile
ile ya USIPOJIPANGA NTAKUPANGA, ukweli umeibiliwa kuwa, Ni kweli, Bwedah,
kabinti Spesho Wa Dully Sykes ni Mke wa Mtu, na ameolewa na Mzungu
Kwa mujibu wa Ndugu wa Hiyali wa
BWEDAH ambaye jina lake halisi ni IRENE, inasemekana kuwa Ni Kweli Bibie huyo
ni Mke wa Mzungu mmoja hivi, huku Vielelezo vya Picha ya Ndoa na Sherehe
zikionekana na kusambazwa kunako Mitandao ya Kijamii hasa Instagram
Aidha ndugu huyo amezidi kumiminika
kuwa, Hivi sasa Ndoa yake inaweza kuvunjika, baada ya Bwedah malanga (Irene)
kuonekana kukolea zaidi kwa Prince Dully Sykes, ingawa awali alishawahi kuaswa
kuwa, afanye Yooote, lakini suala la Ndoa anatakiwa Kuliheshimu.
Hata hivyo inasemekana kuwa, Awali
Bwedah alikuwa hana kitu chochote katika maisha yake, lakini amekuja kufanikiwa
kimaisha baada ya kukutana na Mdhungu huyo.
SIKU YA JUZI, Dully alitupia Picha
ya IRENE ama BWEDAH katika Account yake ya Instagram, na kutunisha kifua kuwa
Huyo ndo KABINTI SPESHO WAKE na ROHO YAKE
EmoticonEmoticon