Rapper kutoka ATL-Atlanta, Nchini
marekani, T.I, amekanusha Vikali tuhuma ambazo watu wamekuwa wakizizusha dhidi
yake kuhusu Kumwandikia Lyrics rapper wa kike IGGY AZAELA
Tuhuma hizo zilianza kuzagaa katika
mwezi ambao tukio la BET lilifanyika, ikiwa ni baada ya NICKI MINAJ kurusha
dongo kuwa, Iggy huenda akawa hana uwezo wa kuandika baadhi ya mistari ambayo
tumekuwa tukiiskia kunako Mikwaju yake ikiwemo FANCY ambayo mpaka hivi leo iko
katika nafasi ya kwanzo kunako BILLBOARDS 100 CHART.
Kwa mujibu wa maelezo ya T.I, amedai
kuwa Bibie huyo kutoka AUSTRALIA na mwenye Miaka 24, ana uwezo mzuri sana hasa
kiakili na kufikilia, kiasi kwamba hawezi kuhitaji T.I mwenyewe amchoree
Mistari ya kuzungumzia kunako Mkwaju wowote…
Pia T.I ambaye amewahi kuhit na
kwaju la TOP BACK na SWING YO RAGS, ameongeza kuwa Iggy ana mawazo yake na
Fikra zake timamu, ambazo anajua ni namna gani atawasilisha kwa Ulimwengu ambao
anautawala hasa katika Muziki anaoufanya.
Hivyop asingeweza kila kitu ambacho
amekizungumza katika Mikwaju yake.
Hata Hivyo T.I ameongeza kuwa,
ingawa ni kweli Wanamuziki wengi hupata Msaada Mkubwa toka kwa Producers wao
ikiwemo hata kubadilisha baadhi ya Mistari na kuiweka sawa, na ni jambo la
kawaida, lakiniIGGY ni mtu mwingine kabisa, na yuko tofauti katika hilo, hasa
uandishi na namna ya kuwasilisha.
MINONG’ONO ya Iggy kuandikiwa Verse
imetawala sana katika akili za watu hivi sasa, jambo ambalo hata Boyfriend wake
ambaye ni mcheza basket Ball, alisema kuwa, tatizo watu wengi wanamuogopa Bibie
huyo, hasa Nicki Minaj, sababu anafanya mambo makubwa sana.
EmoticonEmoticon