MOJA kati ya vitu ambavyo vimewaacha
watu hasa mashabiki wa Busta, ni kauli yake ya kuthibitisha kuwa hivi sasa yeye
na CASH MONEY RECORDS, kila mtu kimpango wake.
Akizungumza katika Moja ya
interview, Busta “Bussa Bus” himself, amethibitisha kuwa ni kweli ametemana na
Record label hiyo, ikiwa ni baada ya kudumu nao kwa muda wa Miaka Minne ambayo
hata hivyo haijakamilika.
Akitoa sababu ambayo wengi pia kuna
Uwezo ikatushtua, ni kitendo cha kukosekana kwa Ubunifu, jambo ambalo lilikuwa
kama Sehemu ya kikwazo hasa kimaelewano
Hata hivyo katika maelezo yake, Busta
amedai amepoteza vitu vingi katika Mchakato wa Kurecord ALBAM moja, ambapo
anasema amempoteza baba yake katika kurecord Albam, amepoteza Mwanga wa Kristo
katika Kurecord Albam, na hata mambo Mengine.
Pia Busta aliongeza ya kuwa, baada
ya kuona mambo hayaendi, na hakuna chochote cha maana alichookifanya akiwa na
Record Label hiyo, aliamua kumfuata Big bos wa CASH MONEY RECORDS, Bird Man, na
Kumwambia kuwa, ni Kweli wamefanya kazi vizuri na anajivunia kuhusu hilo,
lakini hivi sasa anahitaji kufanya kazi vile anavyotaka na anavyohisi inakaa
sawa kwake
BUSTA alitangazwa kuungana na CASH
MONEY RECORDS mwanzoni mwa mwaka 2010, na amefanya nao kazi mpaka hivi sasa
EmoticonEmoticon