Matumizi ya Bangi kwa ajili ya
kujiburudisha yamehalalishwa katika jimbo la Washington nchini Marekani.
Washington ni jimbo la pili nchini Marekani
kuhalalisha Bangi , baada ya Colorado, ambako jimbo hilo linajipatia mamilioni
ya dola kila mwezi kwa kutoza ushuru biashara za Bangi kwa wanaoitumia
kujiburudisha.
Hata hivyo utaratibu wa kuuza bidhaa hiyo
utadhibitiwa ipasavyo katika jimbo hilo.
Ni maduka 25 pekee yaliyoruhusiwa kuuza Bangi
hadi sasa, ingawa maafisa wanaamini kuwa idadi ya maduka huenda ikaongezaka na
kufika miamoja.
Katika sehemu zingine za Marekani, majimbo 23
yanaruhusu matumizi ya Bangi kwa sababu za kimatibabu.
EmoticonEmoticon