WAREMBO 14 kutoka vitongoji mbalimbali vya Mkoa
wa Manyara, wameingia kambini jana kujiwinda na kinyang’anyiro cha kumsaka Miss
Manyara kitakachofanyika Ukumbi wa CCM wilayani Babati na kupambwa na mkali wa
Bongo fleva, Rahim Rummy ‘Bob Junior’, Juni 14.
Mratibu wa mashindano hayo, Akon Clement kupitia
Kampuni ya Mererani Entertainment, aliwataja warembo hao kuwa ni Happy William,
Edna Mushi, Merry Ruta, Rose Evason, Flora Godlizen, Amina Omary, Catherine
Emmanuel, Sabrina Anger, Bertha Fredrick na Samila.
Pia alisema kuwa warembo hao ni kutoka vitongoji
vya Babati, Simanjiro na Mbulu, ambao wameingia rasmi kambini ili kupatiwa
elimu na mazoezi juu ya kinyang’anyiro hicho, hasa ikiwemo kuwajengea uwezo wa
kujiamini na kujithamini.
Aidha alisema kuwa shindano hilo litasindikizwa
na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa Mkoa wa Manyara na msanii maalumu
kutoka jijini Dar es Salaam, Bob Junior.
Akon alisema kuwa shindano hilo limedhaminiwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original,
Kifaru Agrovet, Winners Hotel, Active Classic Fashion, Open University,
Kimweri Sport Wear, Manyara Computer pamoja na Sarafina Lodge.
EmoticonEmoticon