Harakati za Kupiga Vita matumizi ya Madawa ya
Kulevya hasa kwa rika la Vijana, zinazidi kutanuka, baada ya Mwanaharakati RAY
C kujitosa katika SIKU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA.
Kupitia account yake ya Instagram, Ray C ambaye
aliwahi kufanya Vizuri na Track ya SIKUHITAJI, amepost PICHA za maandalizi ya
Banda La taasisi yake ya RAY C FOUNDATION, litakaloonesha shughuli mbali mbali
ambazo anazozifanya, katika Siku Hiyo itakayoadimishwa ALHAMIS ya Tarehe 26
Mwezi wa 6, Jijini Mbeya.
Mgeni Rasmi katika Siku hiyo maalum kabisa
Duniani, atakuwa Dr.Galib Bilal, makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Ray C amekuwa katika Harakati za kupiga Vita
Matumizi ya Madawa ya Kulevya, ikiwa ni Baada tu ya Kusaidiwa Kuepukana na
matumizi hayo ambayo yalikuwa yamemuathiri kwa kiasi kikubwa, na mpaka hivi
sasa ameshasaidia baadhi ya Vijana ambao wataungana Naye huko Jijini Mbeya
katika banda lake.
Kwa Mtazamo wako, Unadhani RAY C atakuwa Kioo cha Watu Wengi Siku Hiyo?
EmoticonEmoticon