REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

SOLANGE-MDOGO WAKE BEYONCE, AMPIGA JAY Z NDANI YA LIFT..FAHAMU CHANZO NA KILICHOTOKEA BAADA YA UGOMVI

2:11:00 AM

BIG ishu ambayo inazunguka hivi sasa kunako Media Mbali mbali Ulimwenguni, Ni Kichapo cha Kimtindo ambacho JAY Z alikipokea kutoka kwa Shemeji ake, SOLANGE KNOWLES, wakati walipotofautiana wakiwa ndani ya Lift ya STANDARD HOTEL
Kwa Mujibu wa Info Ambazo zimeshushwa na Kitengo Chimbua Chimbua, inasemekana Kuwa Tukio hilo lilitokea Wiki iliyopita, walipokuwa katika Shughuli maalum ama tamasha Dogo la MET GALA, lilifanyika katika Hotel hiyo ya Standard, Jijini New York.
Ingawa wengi walikuwa na maswali kuhusu Waliotenda tukio hilo, lakini the Real Ishu Ni kwamba, Video Clip ambayo Imeachiwa na TMZ kutoka kunako SECURITY VIDEO PHOOTAGES, inaonesha wazi kabisa kuwa Muonekano wa watu waliokuwa wakizinguana ndani ya lift hiyo, ni muonekano huo huo wa JAY Z na Shemeji yake SOLANGE, kama ambavyo walionekana wakiwa katika Tukio hilo.

Aidha Video Clip hiyo inamuonesha Solange akimrushia Ngumi na hata Teke Jay Z, huku Beyonce akiwa Pembeni na Mlinzi ndiye alikuwa Msaada wa Kutosha kwa Kuwazuia wawili hao wasiendelea kusuguana za usoni na hata sehemu Nyinginezo.
CHANZO.
Baada ya kupata Mtonyo huo, Kitengo cha Chimbua Chimbua kiliiingia ndani na kukutana na Info kuwa, SOLANGE akijibu swali aliloulizwa kunako Interview na kituo cha Redio cha HOT 97 Nchini marekani, amedai kuwa Hayuko tayari kudharirishwa ama Kuonewa Na Mtu yeyote na yuko tayari kujihami ili kuitetea Heshima yake.

Tofauti na hilo, Solange aliongeza kuwa, pia hayuko tayari kumuona dada yake Beyonce akionewa ama akikosewa Heshima, yuko tayari kutumia Nguvu zake kumlinda na kumtetea.
Kwa mujibu wa Maelezo hayo, ni Dhahiri kabisa kuwa Huenda Jay Z alizinguana na Beyonce, lakini Solange alijumuishwa katika Utetezi na hata Kupewa makavu jambo ambalo lilimfanya Apate hasira na Kumvaa Jigga
BAADA YA UGOMVI..
Yafuatayo ndiyo yaliyotokea Baada ya Ugomvi Huo Kumalizika.
1. Jay Z alionekana Kujiweka sawa wakati akitoka Ndani ya Lifuti huku akionekana kujali sana katika Mashavu yake na Mdomo, na Uso ukiwa Umejaa hasira. Solange alikuwa amefura Balaa na alikuwa Mbele ya Msafara.
2. Beyonce alipost Maandishi kunako account yake ya Instagram, yaliyokuwa yakionekana kumuomba Mungu awasimamie watu wote ambao yuko nao katika mahusiano, awaepushe na Mikwaruzano pamoja na matukio mabaya, huku akisihi Mungu amuepushie Mbali wale wote wasiopenda Mafanikio yake.

3. Utawala wa STANDARD HOTEL ulilaani vikali kitendo cha kuvujisha VCideo Clip Hiyo hasa katika Mitandao ya Kijamii, kwani Ni Ukiukwaji hasa wa kanuni zao katika Kulinda Siri za wateja wao. Pia Umeahidi kumchukulia hatua za Kinidhamu yeyote Yule atakayebainika Kuhusika na Usambaaji wa Phootage Hiyo.
4. BEYONCE na JAY Z walionekana pamoja kwa mara ya Kwanza tangia utokee ugomvi huo, katika Onesho la Mpira wa Kikapu Huko Brooklyn, marekani.
CHECK VIDEO CLIP

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER